MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 ambayo ameyatoa kwa ajili ya jimbo la iringa mjini.
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji
Petter Msigwa amekabidhi madawati hayo 537 ambayo ameyatoa katika jimbo lake
yataweza kuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwasaidia wanafunzi waliokuwa
wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa na baadhi yao
walikuwa wanakaa chini ya sakafu.
Aidha Msigwa katika hotuba
yake ya kukabidhi madawati hayo amewataka viongozi wa manispaa ya iringa na
tabia ya kuhujumu na kuiharibu
miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za
serikali kwa lengo la kuweza kuwasaidia
watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.
“Sipendi kuona wanafunzi
wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa
kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili
kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la iringa mjini”alisema
Msigwa
Naye meya wa halmashauri ya
manispaa ya iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote
ya madawati hivyo hakutakuwa na
changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu.
MADAWATI hayo 537 ambayo
yametolewa na ofisi ya Mbunge wa Iringa Mjini yamegharimu kiasi cha zaidi ya
shilingi milioni 60 yatasambazwa katika kata zote ambapo pia yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea adha
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao walikuwa wanakabiliwa na
changamoto hiyo kwa kipindi cha muda mrefu na hatimaye kuongeza kiwango cha ufaulu.
Lakini tatizo la kupanda na
kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari
katika halmashauri ya manispaa ya iringa lilikuwa linasababishwa na wanafunzi
wengine kujisomea wakiwa wamekaa chini ya
sakafu sambamba na kuwepo katika
mazingira ya miundombinu ambayo sio
rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.
Hayo yamebainishwa na baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya
iringa.
Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige
pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa
sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya
katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la
iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na
adha ya madawati.
“Hapo mwanzoni kwa kweli
hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma
wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa
kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu
kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na
pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema
wanafunzi hao.
Pia walisema kwamba pamoja
na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa
kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na
kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza
kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.
0 maoni:
Post a Comment