Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAFANYABIASHARA ARUSHA WAANDAMANA KUDAI MIKATABA

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamebeba mabango.

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wafanyabiashara wa maduka yaliyoko katika eneo la Stendi Ndogo jijini Arusha wameandamana katika Ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wakidai mikataba ya kupangisha katika maduka hayo yanayomilikiwa na Halmashauri kufuatia mgogoro kati yao na Wajenzi wa maduka hayo.

Kutokana na Sintofahamu hiyo wamelazimika kuandamana nje ya Ofisi za Halmashauri wakishinikiza kupewa mikataba ya upangaji na kudai kuwa wamechoshwa na vitisho wanavyovipata kutoka kwa wajenzi wa maduka hayo ile hali wanalipa kodi kwa Halmashauri.

Prisca  Lema na Witness Riwa ni Wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kuwa licha ya kupewa barua rasmi za kutambulika kama wapangaji wa Halmashauri bado hawajapewa mikataba suala linalowaweka njia panda na kutokujua hatma yao  na kunahatarisha mitaji yao pamoja na mikopo waliyoichukua katika taasisi za fedha.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Hao Josephine Exuper amesema kuwa licha ya tume iliyoundwa na Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutokukamilisha kazi yake na kutoa muafaka tayari wajenzi hao wameanza kujichukulia hatua mikononi na kuwatishia kuwafukuza katika maduka hayo na kudai kuwa wao ni wamiliki halali na si halmashauri.

Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amesema kuwa Baraza la Madiwani tayari limeridhia wapangaji hao kupewa mikataba na Ofisi yake imeweka saini sahihi pekee iliyosalia ili mikataba hiyo iwe tayari ni ya Mkurugenzi wa Jiji kwani uamuzi huo unaungana na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG wa kutaka kuondoa madalali katika upangishaji wa majengo ya serikali ambao unapelekea kupoteza  Bilioni 2.1  ya mapato ya serikali.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha hakupatikana katika Ofisi yake kwa kuwa alikua nje ya Ofisi akitimiza majukumu yake.
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO