Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKUTANO WA WADAU WA WATALII WAFANYIKA ARUSHA









Mwenyekiti wa TATO Wilbroad Chamulo akizungumza na wadau  utalii walipokutana na Mkuu wa mkoa kujifanyia  Tathimini,kuangalia fursa zilizopo katika utalii pamoja na Changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika Utalii.       Picha na Vero Ignatus.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na Wadau wa Utalii katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa( AICC)Katika ukumbi wa Mbayuwayu Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.

Mkutano wa siku moja wa umefanyika Mkoanin Arusha huku wadau w utalii wakiiitaka serikali kuweza kuainisha kodi zote na  kuweka katika mfumo mmoja  ili kuweza kuepuka usumbufu unaojitokeza Mara kwamara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.

Wadau hao wamesema kuwa  kodi hizo waotozwa katika sehemu mbali hususa ni  katika mageti  ambayo  wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja kuufanya nchini hapa



Kwa upande wake  mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) Wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili changamoto na tathimini zinazokabili sekta hiyo .

Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.

"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii wetu kwa ujumla "alisema Chambulo. 

Pia ameitaka serekali  ifutilie na ishughulike na utozwaji Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na geti la wilaya ya Ngorongoro.

"Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao unaimarishwa zaidi"alisema 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na kujadili namna gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa Arusha kwa ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia kukuza mapato na kuwa maradufu zaidi.

Amesema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa  mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.

Ameongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo Mkoani apo.
Mmiliki wa Leopard Safari Faisal Zuhery akichangia jambo katika mkutano huo wa siku moja wa wadau wa Utalii Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.


Katika mkutano huo mambo mambali mbali yaliathimiwa ikiwemo kuitaka serekali na Wadau Wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.
Baadhi ya wadau wa Utalii wakiwa katika kikao cha siku moja kilichoitishwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wakiwa wanasikiliza kwa makini mjadala ulivyokuwa   ukiendelea,ambapo mwisho wakikao walipeana maazimio ya kufanyia kazi ili watakapo kutana tena waweze kuleta mrejesho wa majukumu waliyopeana.     Picha na Vero Ignatus.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO