Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DC MONDULI ATEMA CHECHE KWENYE BARAZA LA MADIWANI


Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Monduli wakiwa kwenye kikwo cha pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli  Idd Hassan Kimanta

Vero Ignatus ...MONDULI.

Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Hassan Kimanta ameliomba baraza la madiwani kumpa usirikiano katika utendaji kazi ambapo ametoa siku 14 kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo  kuhakikisha anakusanya fedha za viwanja vilivyopo Chuo Cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) zaidi ya Shilingi milioni 700 ambazo zitatumika katka miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza kwenye baraza la madiwani monduli na kumuagiza mkurugenzi kuwa fedha hizo zilipwe ndani ya siku 14 na atakayeshindwa kulipa anyang'anywe mara moja na kurudishwa ofisini kwa mkuu wa wilaya na amesema ifikapo jumatano orodha ya watu wenye viwanja hivyo iwasilishwe ofisini kwake, ikiwa na idadi ya waliolipa na ambao bado hawajalipa.

Aidha amemtaka mkurugenzi kubandika matangazo maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kuwataka wananchi wanaomiliki viwanja hivyo kuilipa halmashauri hiyo fedha wanazodaiwa ndani ya siku 14 vinginevyo zikipita siku hizo hatua ya kuwanyang'anya itafuata.

"Nakuagiza mkurugenzi hakikisha unakusanya sh milioni 700 za viwanja vilivyopo CDTI ambavyo vimeuzwa na waliouziwa hawajailipa halmashauri, hadi sasa , wengine wameshajenga na nyumba huku hawajalipa fedha hizo walipe ndani ya siku 14 la sivyo wanyang'anywe alisisitiza Kimanta."

Sambamba na hilo amewataka watumishi wote wa serikali kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi ipasavyo kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya na ikitokea mwananchi anafika kwake wakati viongozi waliopo chini yake hawana taarifa rungu litamshikia kiongozi husika .

Pamoja na hayo amewataka watumishi wote kufika maeneo yao ya  kazi saa moja na nusu asubuhi  siku za kazi na hakuna kuzurura ovyo hadi muda wa kutoka ofisini saa tisa na nusu,huku akiwataka maafisa tarafa kufuatilia katika maofisi mbalimbali ya utumishi wa uma kwani  imeonekana kuna ofisi nyingine watumishi wa uma hawafungui ofisi  kuwahudumia ili wananchi haswa vijiji hadi Kata wilayani humo.

WAKATI HUOHUO:

Mkuu huyo amebainisha kuwepo kwa wanafunzi hewa katika shule za msingi na sekondari katika wilayani Monduli ambapo wanafunzi hewa katika shule za msingi ni 319 ,shule za sekondari 155 huku watoro katika shule ya msingi wakiwa 353 sekondari 115 .

Kutokana na hatua hiyo ya kubainika wanafunzi hewa katika shule za msingi na sekondari serikali imeazimia kuwafukuza kazi walimu 8 wa sekondari na waalimu 6 shule za msingi ambapo tatizo hilo limeisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi  milioni 43.

Katika kuhakikisha swala la elimu linaimarika amesema atahakikisha watoto wakike wanasoma bila kubughudhiwa ,huku alipiga vita ndoa za utotoni,pamoja na ukeketaji kwa watoto wa kike, kwani ni mila potofu katika jamii nainasababisha madhara makubwa kwa watoto wa kike.

"Nawaomba madiwani kwa vile nyie ni wanasiasa suala hili mniachie kwa vile nyie ni  msije kuharibu kura zenu,sijaja kupendwa Monduli wala sihitaji zawadi ya mtu,mimi ndiyo natakiwa niwape ninyi wananchi zawadi ya kuwatumikia ,na nipo tayari kufa kwajili ya kutetea haki yawannchi wa Monduli alisisitiza Kimanta

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO