Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWA FC YATAMBA ARUSHA


TASWA FC NA TASWA SC ZATAMBA KATIKA BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary  na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.


Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa
Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.
Mchezaji nguli wa timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini(Taswa FC),Muhidin Sufiani akichanja mbuga kupenya ngome ya timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)katika mchezo wa fainali ambao Taswa FC walishinda bao 1-0.

Wachezaji wa Netiboli wa Taswa SC na Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)wakichuana vikali katika bonanza hilo ambalo Taswa SC walibamiza bila huruma 30-2

Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa  bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.   

Na Mwandishi wetu
Arusha. Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.
Taswa  FC na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) zilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na waandishi kushindana katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.
Timu ya Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na kichapo katika bonanza hilo  aada ya kuambulia sare ya mabao 2-2. Hata hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya kusawazisha mabao mawili katika dakika sita za mwisho.
Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari  na Utangazaji cha AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.
Taswa FC ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili  ya haraka haraka  kupitia kwa Saidi Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret”  Omary. Martin Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi, Salum Jaba na kipa wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi zote.
Katika mechi ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio , bao la kwanza likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha kona ya Hare Temba na baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia pasi ya Athumani Jabir na Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu na la nne.
Katika mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC, bao la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia kona safi ya Majuto.
Timu ya netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao 30-2 dhidi ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha aliyefunga mabao 22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.
Taswa Queens ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura Abdinoor, Johari William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
Timu zote hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe.  Kwa upande wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote waliondoka na kuku kila mmoja.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya General Tyre alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ambaye alisema kuwa waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya aina mbalimbali ili kuiweka miili vizuri.  
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO