Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Updates: Ally Bananga, Mgombea wa Chadema Kata ya Sombetini anarudisha fomu ya kugombea hii leo

Ally BanangaMgombea wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo Kata ya Sombetini Jijini Arusha, Bw Ally Bananga

********

Taarifa ambazo Blog hii imezipata hivi punde zinaeleza kwamba Ally Bananga amefanikiwa kupata fomu na risiti za Mahakama kwa ajili ya uhalali wa fomu yake ya kugombea inayohitajika Tume ya Uchaguzi baada ya awali kukosa huduma hiyo kwa kile alichoelezwa na Mahakama kuwa hawana risiti ya Serikali. Hii ilikuwa ni katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso Jijini hapa.

Ilimlazimu Ally Bananga na watu wake kuondoka na kwenda Mahakama ya Wilaya ya Sekei ambako nako hakufanikiwa na kisha kurudi tena Maromboso ambako ndio hivi punde tu ameweza kufanikisha.

Muda huu Bananga na msafara wake wanaelekea Ofisi ya Wilaya kurudisha fomu za mgombea wa Chadema rasmi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO