Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ufafanuzi wa Wakili Peter Kibatala kuhusu Kesi ya Zitto dhidi ya Chadema

kibatala na zitto

Peter Kibatala, Wakili na Mkurugenzi wa Sheria,Katiba na Haki za Binadamu CHADEMA (kushoto) akizungumza na Wakili wa Mh Zitto Kabwe, Bw Albert Msando.Picha ya Maktaba kwa hisani ya Dullonet

**********************************
Baada ya kupokea message na wito mbali mbali kuhusu haja ya kutoa ufafanuzi kuhusu yaliyojiri katika Shauri la Zitto Zuberi Kabwe Vs Baraza la Wadhamini,CHADEMA na Katibu Mkuu CHADEMA.

Shauri limefunguliwa likiwa na sehemu Kuu mbili,Shauri ama Case ya Msingi,na maombi madogo ya Zuio la muda.

Katika Shauri Kuu Muombaji anaiomba Mahakama Kuu kwa amri tatu;1.Chadema izuiwe kujadili suala la uanachama wake mpaka pale Atapopewa nakala za mwenendo na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua nafasi za Uongozi, na Rufaa yake dhidi ya Uamuzi huo kusikilizwa na Kamati Kuu ya Chadema.2.Chadema iamuriwe kuitisha Baraza Kuu ili kujadili Rufaa hiyo.

Msingi wa Madai ni kwamba wakati mchakato wa Rufaa haujakamilika,na wakati haja pewa nakala za mwenendo na uamuzi wa kumvua nafasi za Uongozi,ameitwa na Kamati Kuu kujadiliwa kuhusu Uanachama wake.

Katika Shauri dogo lililotolewa uamuzi Jana,Muombaji aliomba amri ya Zuio ili Kamati Kuu au Chombo kingine cha Chadema isijadili Uanachama wake mpaka Shauri la msingi litakaposikilizwa,na kutolewa Uamuzi na Mahakama Kuu.

Shauri lilifunguliwa tarehe 2/1/2014,na siku hiyo hiyo Mimi na Wakili Tundu Lissu tulitoa mapingamizi Matatu dhidi ya Maombi;1.vifungu vya Sheria vilivyotumika havikuwa sawa.2.hati ya kiapo Ina mapungufu.3.mahakama haina mamlaka kujadili migogoro ya vyama vya siasa,na taasisi zenye tabia ya uhiari.

Mahakama ilikataa mapingamizi yote Matatu katika uamuzi wake wa tarehe hiyo 2/1/2014,uliosomwa Saa 12 hivi za jioni.

Pande zote tukabaliana kwamba maombi madogo yasikilizwe tarehe 3/1/2014,na kwamba wadaiwa Walete hati ya kiapo kinzani Saa 2.30 asubuhi ya tarehe 3/1/2014 ili Saa 3 asubuhi hiyo tusikilizwe maombi Yale madogo niliyotaja hapo juu.

Mimi Kama Wakili nikala kiapo na kutoa hati ya kiapo kinzani kwani kwa mazingira Yale ya uharaka isingekuwa rahisi kuwapata wadhamini wa chama ili watoe hati ya kiapo usiku au asubuhi mapema na kuwahi Mahakama.

Cha msingi zaidi ni kwamba Mawakili tumepewa na Chana mamlaka kamili kuhusiana na Shauri.

Wakati wa usikilizaji Mahakama yenyewe (suo mottu) ikazitaka pande zote ziieleze Mahakama Kuu iwapo ni sahihi Wakili kula kiapo kwa niaba ya mteja katika Shauri Kama lile.

Pande zote ziliieza Mahakama kwamba ni sahihi,ingawa Wakili Msando alipinga aya ya nne ya hati ya kiapo kwa sababu za kisheria.

Kisha tukajadili maombi yenyewe. Hoja zetu zikawa kwamba Muombaji amepewa nafasi ya kusikilizwa kwa kuitwa Kamati Kuu,pia tukasisitiza Mahakama haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya taasisi Kama Vyama vya siasa.

Katika uamuzi wake wa tarehe 7/1/2014 Mahakama imeamua kwamba pamoja na pande zote kukubaliana kwamba ni sahihi Wakili kula kiapo kwa niaba ya mteja anayemuwakilisha Mahakamani katika mazingizira ya Shauri lile,haikuwa sahihi.

Ilikubaliana pia na Wakili Msando kwamba aya ya nne Ina taarifa ambazo ilitakiwa zitolewe na mtu aliyekuwa katika Kikao cha Kamati Kuu,na si Wakili.

Ikaamua kukifuta kiapo.

Mahakama ikaamua pia kwamba mleta Maombi anastahili Zuio la muda ili suala la Uanachama wake lisijadiliwe mpaka Case ya msingi itaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Case ya msingi inaendelea,na Chadema kupitia sisi mawakili wake inaandaa utetezi ambao kwa mujibu wa Sheria unatakiwa Mahakama ifikapo tarehe 23/1/2014.

Kuhusu suala la mwenendo wa Kikao cha Kamati Kuu na kuitisha Baraza Kuu,Chama kitazungumza kwa namna na muda itaoona unafaa.’’

Peter Kibatala,

Wakili na Mkurugenzi wa Sheria,Katiba na Haki za Binadamu;CHADEMA.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO