Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

PICHA YA BEYONCE ILIYODAIWA KUMKUFURU YESU KRISTO

Mtandao wa hip hop morning umeelezea jinsi msanii wa muziki wa majuu maarufu kama "Beyonce" alivyoonekana kuwakela watu wengi nchini Marekani hasa wale wakristo.

Mwanadada Beyonce, inasemekana juzi kati tarehe 30 ya Desemba 2013 alitupia picha hiyo hapo juu inayomuonesha Beyonce akiwa amekaa mbele ya meza kubwa, ambapo nyuma yake kuna picha ya wanafunzi wa Yesu wakiwa wameketi pamoja  naye.

Lakini Beyonce ameonekana kuziba nafasi ya Yesu Kristo katika picha hiyo, kitu ambacho kimezua utata mkubwa mno kuwa, huenda Beyonce amejifananisha na Yesu au anajaribu kujifanya yeye ndio yesu au amepindua utawala wa Bwana Yesu Kristo.

Kitendo hicho kimewakera wakristo wengi duniani, kwa msanii huyo kutoheshimu Imani za Wakristo. Hatahivyo wengine wameibuka na mtazamo mwingine kuwa, huenda mwanamuziki huyo akawa naonyesha nembo za mpinga Kristo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

rehema said...

Hio ni picha tu ya watu walio igiza kama Yesu na wanafunzi wake sio yesu huyo na wala sio wanafunzi Wa yesu nyie mbona wavivu Wa kufikiri?

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO