Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

James Ole Millya Auaga Ukapera Rasmi kwa Kuoana na Bi Janeth! Hogereni Maharusi.

Kamanda wa Chadema Arusha, James Ole Milya akiwa na sura ya tabasamu na mkewe Janeth jioni ya Mei 3, 2014 katika ukumbi wa Botanical Garden- Sakina ilipofanyika tafrija kusindikiza harusi yao. Blog hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa waili hao na kuwatakia kila lililo jema katika maisha yao ya ndoa hadi uzee wao. Mungu Awabariki sana James&Janeth

Kutoka kushoto, Msanifu Majengo Dudley Mawalla wa MD Consultancy iliyosanifu Jengo la PPF Plaza linalijengwa mkabala na Kibo Palace Hotel, anafuata Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freeman Mbowe na kisha Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na mkewe wakiwa wameshika glass zao kwa ajili ya kutakiana heri na maharusi.

IMGP0046

Maharusi wakifurahi na marafiki. Hapa ni picha ya pamoja na mdau Daniel Urioh

Mbunge Lema akilishwa keki na maharusiMsanii wa Injili Christina Shusho akitoa burudani ukumbini hapo

Msanii wa Kimataifa toka Kenya, Solomoni Mukubwa akitoa burudani

Maharusi wakiimba sambamba na msanii Shusho (haonekani pichani) huku MC OJ kutoka Kenya akifanya yake

***************************************

Sherehe ya kusindikiza harusi ya James Ole Millya na mkewe Bi Janeth ilikuwa ya kipekee kwa namna mbalimbali ukiachana na idadi kubwa ya watu waliohudhuria.
Ni sherehe iliyokuwa na mbwembwe za kila namna na vikorombwezo chungu tele.

Utaani wa kisiasa baina ya Chadema anakotoka bwana harusi na CCM anakotoka bi harusi ulikuwa ni kivutio tosha kwa waliohudhuria. Makundi ya vyama vyote yakiwa na viongozi wao wakubwa yalikuwa yakitambiana kwa kushangilia kila walipopata fursa toka kwa MC. Mabaraza ya vijana kwa vyama vyote ndio yaliyotia for a kwa pande zote katika kutambiana. Huku CCM wakiimba “CCM..CCM..” wenzao wa Chadema walikuwa wakionyesha ishara ya vidole vitatu na kuimba “UKAWA…UKAWA” kila alipotambulishwa kiongozi wao ama kuitwa kufanya jambo fulani. Bavicha Arusha waliongozwa na Mwenyekiti wao Noel Olevaroya na Katibu Glory Kaaya.

Kulikuwa na idadi kubwa ya viongozi wa kitaifa na kisiasa. Alikuwepo Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni mbunge wa Hai, Mh Freeman Mbowe bila kumsahau Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na Mh Kihwelu kwa Upande wa Chadema. Walikuwepo pia Mwenyekiti wa CCM  Arusha Mh Olenangoye na Mbunge Viti Maalum CCM Mh Catherine Magige. Madiwani Kessy wa Kaloleni, Ally Bananga wa Sombetini na Msofe wa Daraja mbili wote kupitia Chadema walihudhuria.

Viongozi wa kiserikali alikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja Kota, bila kumsahahu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini John Mongela. Mbunge wa Simanjiro anakotokea James Millya, Mh James Ole Sendeka hakuonekana ukumbini hapo pamoja na kuwa alialikwa. Blog hii iliweza kufahamu kuwa takribani watu 10 walialikwa kutoka katika kila kijiji cha Wilaya ya Simanjiro, pengine ndio sababu iliyopelekea James kupewa zawadi ya ng’ombe wengi mno kutoka kwa jamaa zake Maasai.

Upekee haukuishia hapo tu kwani kwa upade wa washereheshaji walikuwepo nguli wawili wa fani hiyo, MC OJ (Alezander Josephat Ole Midimu Sirkion) ambaye ni mchekeshaji kutoka Kenya na aliwahi kuwa Kampeni Meneja wa Raila Odinga, bila kumsahahu Godwin Gondwe kutoka Tanzania.

Burudani haikuishia hapo kwani nyimbo za injili ziliimbwa na wasanii Christina Shusho kutoka Tanzania na Solomoni Mukubwa kutoka Kenya ambao kwa pamoja walikonga nyoyo za wahudhuriaji vilivyo.

Kali kuliko ni rundo la zawadi kubwa kubwa kwa Bwana Harusi. Ngugu zake jamii ya kimasai na wazazi walitoa jumla ya ng’ombe zaidi ya 200 na ekari kadhaa za shamba. Wazazi walezi nao walitoa sehemu ya hisa za kampuni yao na kuahidi kumpatia James sambamba na ofa ya tripu ya wiki mbili nchini Sweden, bila kusahahu kiwanja cha kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya Kisongo nyuma ya uwanga wa ndege.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO