Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Joshua Nassari aibua simanzi katika kumbukizi ya kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema Usa-River kwa kuchinjwa shingo

Nassari Mei 4 2014

Jana Mei 4, 2014 wakazi wa Usa-River hususani wananchi wanaounga mkono harakati za Chadema katika kupigania haki za raia walijikuta katika hali ya simanzi kubwa baada ya hotuba mfululio zilizowakumbusha tukio baya ya kuuawa kwa aiyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa-River, Marehemu Samsoni Mbwambo, aliyeuwawa miaka miwili iliyopita kwa kuchinjwa shingo kwa nyuma na kilichoelezwa kuwa msumeno wa mbao jirani na yumbani kwake.

Ulikuwa ni mkutano wa Kumbukizi ya kuuawa kwa Mbwambo lililofanyika katika viwanja vya Ngaresero. Walianza viongozi wa Wilaya na mitaa wa chama hicho kuelezea masononeko yao na hali ilivyokuwa na baadae kuhitimishwa na Mbunge Joshua Nassai ambaye hotuba yake ilikuwa yenye kutia simani sana.

Nassari alitumia muda mfupi wa hotuba yake kukumbusha kisa halisi kilichosababbisha mbwambo kupoteza uhai akiwa ni mtu aliyejitolea kwa kumaanisha kupiganaia mabadiliko ya Arumeru Mashariki. Nassaei alisema Mbwambo akiwa Mwenyekiti wa Chadema Usa-River alifuatwa na watu wa chama kilichoshindana sana na Chadema kwenye uchaguzi huo wakimtaka awasaidie kufanya hujuma kwa kuharibu fomu ya Nassari ili awekewe pingamizi na mpizani wake wakati huo apite bila kupingwa.

Akiendelea kusimulia, huku ukimya ukitawala viwanja vya Ngaresero, Nassari alisema kuwa Bw Mbwambo alipokea fedha walizompatia kwa kazi hiyo lakini hakuweza kutekeleza na badala yake akatoa taarifa kwa viongozi wa Chadema. Baadaye kamapeni zikaanza, wakamtegemea pia kutoa siri lakini hakufanya hivyo mpaka uchaguzi ukafanyika na Joshua Nassari kutangazwa mshindi. WIki mbili baadaye, baada ya Mbwambo kuhudhuria kuapishwa kwa Nassari Bungeni Dodoma ndio alifikwa na mauti kwa kuuawa na watu ambao wameelezwa kuwa walitumwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na kwamba baada ya kuuawa kwa Mbwambo viongozi wengine wa Chadema akiwemo Nassari na Mwenyekiti wa Wilaya wanadai kupokea simu za vitisho zilizowaelekeza kuwa zamu yao ilikuwa inafuata.

Watuhumiwa wa mauaji walikamatwa lakini wakatoroka katika mazingira ya kutatanisha mbele ya askari wakitolewa Mahakamani Arusha kurudishwa gerezani, jambo lililoelezwa katika kumbukizi hiyo kwamba lilitokana na watu hao kuwa tayari kuwataja waliowatuma kufanya ukatili huo.

Nassari aliuambia umati wa wananchi waliojitokeza kuwa Bw Mbwambo aliuwawa kwa kupigania watu wake na kwamba alikuwa ni mtu aliyejitolea kwa kumaanisha kupigania mabadiliko ndani ya Arumeru na Usa-River kwa ujumla. Nassari anamsomesha Sekondari binti mmoja wa marehemu, na katika mkutano huo aliendesha harambaee ya kumchangia mjane wa marehemu na watoto wake.

Awali Katibu wa Mbunge Nassari, Bw Toti Ndonde alitoa taarifa ndefu na ufafanuzi wa ahadi na mambo mbalimbali ambayo Nassari amekwishatekeleza yakihusu kero za maji, elimu na barabara pamoja na matumizi mabaya ya fedha za Halsmahauri. Akahitimisha kwa kuaga wananchi hao na kuwashukuru kwa muda wote waliokuwa pamoja wakishirikiana vyema na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Katibu mwingine atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, japo hakueleza sababu za kung’atuka.

Nassari na timu yake ya chama Wilaya wamekuwa wakifanya mikutano takribani mitatu kila mwisho wa wiki kuzungumza na wananchi na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika Kata zote za Jimbo la Arumeru Mashariki.

Kituko
Mkutano ukiwa unaendelea, alikatiza mtu mmoja aliyevalia kofia ya chama tawala CCM, wananchi wote waliacha kufuatilia mkutano na kuanza kumzomea kwa nguzu kiasi cha kufanya mzungumzaji ashindwe kuendelea.

Samson MbwamboMarehemu Mbwambo enzi za uhai wake , alipokweda Dodoma kushuhudia kuapishwa kwa Joshua Nassari

marehemu MbwamboTunaomba radhi kwa picha hii; namna Bw Mbwambo alivyokuwa amechinjwa

Nassari na SeriaNassari akiwa benchi kuu na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema kabla ya kupanda Jukwaani kuzungumza na wananchi na kisha kuhitimisha mkutano kwa harambee kumchangia mjane wa Mbwambo.
Nassari

Nassari

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO