Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAJINA YA WALIOMALIZA FORM SIX MWAKA 2014 WANAOTAKIWA KWENDA KURIPOTI JESHINI KWA MAFUNZO HAYA HAPA

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2014.
  • AWAMU YA KWANZA; VIJANA 20,000 WATARIPOTI KWENYE MAKAMBI YA MAFUNZO YA JKT KUANZIA TAREHE 01 JUNI 2014 NA KUANZA RASMI MAFUNZO YAO TAREHE 08 JUNI 2014 NA KUMALIZA TAREHE 04 SEPTEMBA 2014. ORODHA YAO ITAANZA KUONEKANA KWENYE WEBSITE YA JKT TAREHE 11 MEI 2014 KUANZIA SAA NNE (4) ASUBUHI.

  • AWAMU YA PILI; VIJANA 14450 WATARIPOTI KWENYE MAKAMBI YA MAFUNZO YA JKT KUANZIA TAREHE 11 SEPTEMBA 2014 NA KUANZA RASMI MAFUNZO TAREHE 18 SEPTEMBA 2014 NA KUMALIZA TAREHE 17 DESEMBA 2014. ORODHA YAO ITAANZA KUONEKANA KWENYE WEBSITE YA JKT TAREHE 15 MEI 2014 KUANZIA SAA KUMI (10) JIONI.

  • KIJANA YEYOTE MWENYE ULEMAVU UNAOONEKANA ARIPOTI KATIKA KAMBI YA MAFUNZO YA RUVU JKT (832 KIKOSI CHA JESHI).

  • VIJANA WOTE WANATAKIWA KUWA NA VYETI VYA KUMALIZA KIDATO CHA SITA ( LEAVING CERTIFICATE).

  • INASISITIZWA VIJANA WARIPOTI KWENYE MAKAMBI WALIOPANGIWA NA SIO KUJA MAKAO MAKUU YA JKT.

BOFYA HAPA CHINI KUTIZAMA MAJINA KWENYE VIKOSI MBALIMBALI


IMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO