Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) WAKITOA SEMINA KWA WANAHABARI NA BLOGA WA ARUSHA

DSC09849

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent MungI akitoa mada katika Semina ya siku moja, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa ASILI YETU TANZANIA BLOG Bw. Victor Machota akiwa na Gadiola Emanuel mwenyekiti wa Arusha Bloggers Associations na Mkurugenzi wa WAZALENDO 25 BLOG katika Semina ya siku moja iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Bosi mzito wa Blogu hii akifuatilia jambo kwa makini katika seminahiyo

Mwanahabari toka Radio 5 Fm Bw. David Rwenyagira akisikiliza kwa makini katika Semina ya siku moja, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Kushoto ni Woinde Shizza ,Kiko ,Jane Edward na anaecheka kwa furaha ni Philbert Rweyemamu katika Semina ya siku moja ya wanahabari, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Innocent Mungi kutoka TCRA akitoa semina katika maswala mbalimbali yahusuyo mawasilioano nchini.

Wanahabari mbali mbali wakisikiliza kwa umakini Semina ya siku moja ya wanahabari, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Meneja wa Mawasiliano wa TCRA akipata Zawadi ya Shuka la Kimaasai na Mkanda kutoka kwa Arusha Press Club mara baada ya kutoa mada katika Semina ya siku moja ya wanahabari, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

TRCA kupitia Bw Mungi waliwaomba sana wanahabari na bloga wa Arusha kutumia taaluma yao kusaidia kuielimisha jamii ya kitanzania kuhusianna na matumizi sahihi na bora ya mawasiliano ili yawe na tija zaidi. Kwamba si nia ya TCRA kuingilia uhuru wa wananchi katika kuwasiliani lakini ni vyema kuelimishana ili matatizo mengine yanaweza kuondoka kwa elimu kuongezeka.

Mweka hazina wa Arusha Press Club na Mkurugenzi wa Jamii Blog Bi. Pamela Mollel akitoa zawadi kwa Meneja wa Kanda ya kaskazini Bi. Eng. Annette E. M. Matindi (hayupo pichani) akipokelewa na mwakilishi toka TCRA Bw. Julius Felix katika Semina ya siku moja ya wanahabari, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Arusha Press Club Bw. Cloud Gwandu akitoa shukrani kwa niaba ya wanahabari waliohudhuria katika Semina ya siku moja ya wanahabari, iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Arusha Press Club(APC) leo 5 Sept. 2013 Olasiti Garden Jijini Arusha.

Bw Innocent Mungi akivalishwa mkanda wa kiasili kukazia rubega na Mweka Hazina wa klabu ya waandishi wa habari Arusha, Bi Pamella Mollel.

Ramani ya mkongo wa mawasiliano

Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Semina, kutoka kushoto ni Julius Felix (TCRA) , Seria Tumainiel ( Arusha 255 Blog ), Bw. Innocent Mungy (TCRA) ,Victor Machota (ASILI YETU TANZANIA Blog) ,Gadiola Emanuel (WAZALENDO 25 BLOG) na Woinde Shizza (LIBENEKE LA KASKAZINI). Baadhi ya picha; na Gadiola Emanuel.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO