Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Taswa FC ya Dar es Salaa Yanogesha Bonanza la Wanahabari wa Jijini Arusha leo

Kikosi cha Taswa Fc kutoka Jijini Dar es Salaam kilichoshiriki mechi mbalimbali kwa mtindo wa ligi katika Bonanza la Wanahabari na Wadau wa Habari Jijini Arusha. Bonanza hilo limeandaliwa na Taswa Arusha kwa udhamini wa TBL, TANAPA, Mega Trade, Coca Cola Zero, Pepsi.

Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoani Arusha, Bw Musa Juma jumla ya timu 12 zilitarajiwa kushiriki, kukiwa na michezo mingine kama kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira wa pete, bila kusahau burudani ya muziki kutoka kwa bendi iliyoalikwa na dj

Baadhi ya timu zilizo shiriki katika tamasha hili la nane kuandaliwa na Taswa Arusha, ni pamoja na Taswa Fc ya Jijini Dar es Salaamu ambapo, Taswa Arusha ambao ni wenyeji wa bonanza.

Wengine ni timu ya ORS Fm ya Manyara, timu ya Sunrise fm, Radio five, AJTC, pamoja na timu ya TBLambao ni miongoni mwa wadhamini.

Winga wa Taswa FC ya Dar akipiga mpira wa adhabu ndogo kuelekea langoni mwa timu ya Redio Five ya Jijini Arusha

Wachezaji wa Taswa ya Dar wakisalimiana na wenyeji wao timu ya Redio Five

Taswa Fc ya Dar wanakwenda mapumziko katika mechi ya kwanza

Wakati wanaTaswa toka Dar es Salaam wakiwasili viwanja vya General Tyre, Jijini Arusha.

Shaffih Dauda kabla ya kuingia dimbani

DSC00019Kikosi kamili cha Taswa Fc ya Dar es Salaam

Baadhi ya wachezaji wa AJTC (Chuo cha habari Arusha)

Timu za AJTC (wenye njano) wakiwa katika ukaguzi na timu ya Arusha One redio. Arusha one waliibuka washindi kwa 2-1 katika mechi hii.

Wachezaji wa Arusha One wakipatiwa maelekezo na waratibu wa Bonanza kabla ya mechi kuanza katika kusisitiza mchezo wa upendo na amani.

Mashabiki wa Arusha One Fm wakifuatilia mpambano

Timu ya ORS Fm toka Manyara (wenye njano) pamoja na timu ya Sunrise Fm ya Jijini Arusha kabla ya mpambano wao ulioisha kwa Sunrise kuibuka washindi kwa goli 2 dhidi ya 1 la ORS.

Vyombo vya muziki vikiwa vinawekwa sawa mapema asubuhi katika viwanja hivyo.

Katibu wa Taswa Arusha, Mussa Juma (mwenye kofia) akichambua majina ya baadhi ya wachezaji na waratibu wenzake wa Bonanza hilo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO