Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

PICHA: MKUTANO WA DR SLAA WASHINGTON DC

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa leo Jumapili Sept 22, 2013 aliongea na Watanzania wa DMV na vitongoji vyake kuhusu mstakabali mzima wa Tanzania, kisiasa, kiuchumi na huku akigusia mali asili na utalii, kusafirishwa kwa wanyama nje ya nchi kinyemela.

Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi akizungumuza na kueleza historia ya tawi la CHADEMA DMV lilivyoanzishwa kabla ya kumkaribisha katibu wa tawi DMV, Bwn. Liberatus Mwang'ombe.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu wa CHADEMA DMV Bwn. Liberatus Mwang'ombe.

Bi. Josephine Mshumbuzi akiongea na wanaDMV kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere.

Mama Leticia Nyerere akipeana Mkono na Mchungaji Materu katika Mkutano wa Chadema DMV uliohutubiwa na Dr Slaa

Pichani ni baadhi ya Wakazi wa Washington DC (DMV) Waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa.

PICHA ZOTE NA CHADEMA BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO