Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MSIBA BONGOFLEVA: YP WA TMK AFARIKI DUNIA

 

Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa leo katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.

“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema…

Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa leo katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.

Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.

“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.

“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”

http://www.globalpublishers.info/)

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO