Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KONGAMANO LA TANO LA KIMATAIFA KUJADILI MATUMIZI YA NISHATI ITOKANAYO NA JOTO ARDHI KATIKA NCHI ZA AFRIKA ZINAZOPITIWA NA BONDE LA UFA LAFANYIKA ARUSHA, DR BILAL MGENI RASMI.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo.

  Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili ya kabila la wamasai wakati akiondoka katika Ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO