Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SHINDANO LA MODEL OF TOURISM KUFANYKA KESHO NOVEMBA 22 JIJINI ARUSHA

SAM_1036Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiongea na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha ambapo waliweza kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo

SAM_1055 Meneja Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha

SAM_1029Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo Samdia Charles

SAM_1076

Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha

SAM_1065

Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa akiwa anawasikiliza washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha (hawapo pichani)ambapo aliwataka washiriki hao kutumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa ndani

SAM_1073Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akipata utambulisho kutoka kwa washiriki wa shindano hilo

SAM_1071Washiriki wakipata picha ya pamoja nje ya jengo la makao makuu ya TANAPA jijini Arusha

SAM_1068

SAM_1042Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiwa anatoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania

Washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania wametakiwa kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kutembelea hifadhi za Taifa

Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa ,jana wakati washiriki wa shindano hilo walipopata fursa ya kutembelea makao makuu ya TANAPA jijini Arusha

Bw. Mussa aliwataka washiriki hao kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayo pelekea idadi ya watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi za Taifa

Alisema kuwa ipo haja kwa watanzania kuona utalii ni sehemu ya starehe ambayo unaweza kujifunza hata ukiwa na familia yako tofauti na starehe zingine

Naye Maratibu wa shindano hilo Samdia Charles alisema lengo la kuanzishwa kwa shindano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya nchi yetu kimataifa kupitia maonyesho ya mavazai kama vile new York fashion week,Paris fashion week na Victoria’s secret fashion show

Aidha alisema kuwa katika shindano hilo washiriki wametoka katika mikoa mbalimbali ya Dar es saam, Arusha,Iringa,Mbeya,Manyara,Singida,Kilimanjaro,Tanga,Tabora,Dodoma na Mwanza
Shindano hilo lilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu kuna jumla ya washiriki 19 kati yao 16 ni mabalozi wa hifadhi za taifa na shindano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 22 novemba 2014katika ukumbi wa triple A jijini Arusha

 

CHANZO: PAMELA MOLLEL

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO