Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWANANCHI HUYU WA SOKONI 1 ARUSHA ANAHITAJI MSAADA WAKO!

Steven John anayesumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tumbo. AMETOKA WAPI?

John ni mkazi wa Kijiji cha Sokoni One, mkoani Arusha, amekua akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa kipindi cha miaka miwili bila kupata nafuu na hali yake inazidi kubadilika kila mara ingawa ametakiwa na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kufanyiwa upasuaji wa pili baada kufanyiwa hivyo huko nyuma.

Mgonjwa huyu anazunguka huku na kule kutafuta fedha bila mafanikio na kwa sasa anawaomba watu wenye huruma wamchangie ili akamilishe tiba yake.

FAMILIA INAISHIJE?

“Nina familia ya mke na watoto nane, walikuwa wakiishi kwa kunitegemea lakini kwa kipindi cha miaka miwili sasa wamekosa msaada wangu, kwani nimekuwa nikizunguka hospitali kadhaa huku nikiwa na mke wangu kutafuta matibabu lakini tunakumbana na vikwazo vingi kikiwemo cha ukosefu wa fedha.

“Jambo hilo linanifanya niwe na mawazo mengi sana ya kumtaka Mola aichukue roho yangu, kwani nimeanza kuchungulia kaburi kuliko kuisumbua familia yangu inayoteseka kwa kukosa matunzo nami kuteseka kwa maumivu makali, nimekuwa ombaomba hapa mjini ili nipate fedha lakini hakuna mafanikio.

Muonekano wa sehemu za kutolea haja kubwa na ndogo. SOMA ZAIDI>>>

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO