Katika kile kinachoonekana kuwapo kwa hila ama jambo lisilo sawa katika Katiba inayopendekezwa, Jaji Mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba amejikuta katika wakati mgumu na kudhalilishwa wakati wa mdahalo huru kuhusu maswala ya Katiba Mpya
Mdahao huo uliokuwa unarushwa live kupitia runinga ya ITV kutoka Ubungo Pearl ulikuwa na mada isemayo "Katiba Mpya-Maoni ya Wananchi na Katiba Inayopendekezwa" ulianza kwa amani na utulivu lakini ulikuka kuvurugika baada ya vijana wanaodaiwa kutumwa na viongozi wa CCM kuingilia kati na kuanzisha vurugu kubwa zilizopeleke mdahalo huo kuahirishwa.
Kiongozi wa UVCCM Paul Makonda analaumiwa kwa kuwa kinara wa vurugu hizo ambapo anadaiwa kuthubutu kumrushia chupa Jaji Warioba ambaye aliokolewa na wanausalama.
Wadadisi wa mambo wanatafsiri tukio hili la aibu kama sehemu ya muendelezo wa CCM kujaribu kuzuia ukweli mwingine kujilikana kuhusu Katiba Mpya ambayo yapaswa kuwa ni Katiba ya wananchi wote bila kubagua kundi lolote.
Itakumbukwa kuwa Katiba Inayopendekezwa imelazimishwa kupatikana kwa kukiuka baadhi ya taratibu na hata kufoji kura za maamuzi.
Picha hizi ni baadhi ya matukio wakati wa vurugu hizo.
0 maoni:
Post a Comment