Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana umetekekeza kabisa soko la bidhaa za utamaduni maarufu kama “Maasai Market” lililoko mkabala na ofisi za CCM Wilaya ya Arusha Mjini. Moto huo uioanza majra ya saa tano kasoro usiku umeunguza vibanda vyote eneo hilo na kila kilichokuwemo. Baadhi ya wamiliki wa biashaa hizo wameangua vilio huku baadhi wakizirai na kukimbizwa hopsitali baada ya kupata mshtuko kutokana na kilichotokea.
Pichani juu ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwa katika hali ya mshangao kwa kile anachokishuhudia.
Jambo la kushangaza zaidi, Makao Makuu ya Idara ya Zimamoto kwa Jiji la Arusha yako kiasi cha mita mia mbili tu kutoka eneo la tukio lakini hawakuweza kutoa msaada wa kuzima moto huo ambao unaelezwa ulianzia mabanda ya nyuma na kusogea mbele kwa kasi sana.
Baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii wamehoji uwepo wa Idara hiyo ya Zimamoto kama hakuna kazi wanayofanya hapa Jijini.
Baadhi ya wamama wafanyabiashara ya vinyago na mapambo ya asili pamoja na nguo za kiutamaduni wakijadiliana mawili matatu
Mh Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini akiwafariji baadhi ya wahanga
0 maoni:
Post a Comment