Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MH.LOWASSA ALIPOZINDUA HELKOPTA YA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa kwenye kwenye jukwaa kuu na mwenyeji wake,Ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima (kushoto),Kawe jijini Dar es Salaam jana.Wengine pichani ni Askofu Eliud Isanje (wa pili kulia) na Mchungaji Elifuraha Laswai (kulia).

Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Helkopta iliyonunuliwa na Mchungaji huo kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Helkopta itakayotumiwa na Mchungaji huyo katika kazi zake za kiroho,hafla hiyo imefanyika jana kwenye viwanja vya Kawe,Jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na baadhi ya wachungaji waliohudhulia kwenye hafla hiyo.

wakielekea kwenye uzinduzi rasmi wa Helkopta.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mtoto wa Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiiingia ndani ya Helkopta hiyo kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za kihuduma ya kiroho,itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Edward Lowassa akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.

Helkopta iliyozinduliwa ikipaa kuondoka uwanjani hapo na baadae kurudu mara baada ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakati akimuelezea kuhusu vitabu vyake alivyoviandika kabla ya kuvizindua rasmi.

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kwenye vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto)

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyesha moja ya vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto) wakati alipovizindua rasmi jana

Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO