Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: NAMNA MWENYEKITI WA CHADEMA ALIVYOFUNIKA KATIKA MIKOA YA KIGOMA NA KATAVI

 

Akinamama wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakicheza ngoma ya asili, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), baada ya kuwasili kijijini hapo, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Wananchi wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwakabidhi kadi za Chadema waliokuwa viongozi wa CCM wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katija jimbo la Mpanda Vijijini, baada ya kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM 

Waliokuwa viongozi wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga kupitia CCM, wakionyesha kadi zao kabla ya kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipojiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijiji hapo

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO