Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MATUKIO ZAIDI - MDAHALO WA KUJADILI KATIBA ULIOVUNJIKA NA JAJI WARIOBA KUTOLEWA UKUMBINI

Jaji Joseph Warioba akitoa mada.

Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam.

Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.

Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.

Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.

Vijana wakiwa na mabango.

Mabango yakiwa juu.

Vujo zinaanza.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.

Baadhi ya viti vilivyovujwa.

Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.

Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.

Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.(Picha zote na Francis Dande)

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO