Hali ya taharuki iliibuka ghafla Bungeni Ddodoma usiku huu baada ya UKAWA na wabunge baadhi wa CCM kugoma kuendelea na mjadala wa Bunge wakishinikiza Waziri Muhongo awajibishwe....
Hali hiyo ilitokea baada ya kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe kusimama na kumtuhumu Spika wa Bunge kujaribu kuwakumbatia wezi wa Pesa za Escrow, akijaribu kulazimisha mapendekezo ya Bunge kutokuwa na maneno ya kumtaka Rais awafukuze uwaziri, kwa wakati huo ilikuwa ni zamu ya Waziri Muhongo na badala yake iwe tu ushauri kwa Serikali iamuamue cha kuwafanya.
Spika alijaribu kumsihi Mh Mbowe aendelee kuzungumza lakini Mbowe akawa amesimama na wengine nao wakasimama na kuonekana wakipanga vitu vyao kama wanataka kutoka lakini hawakutoka na kuendelea kusimama wote.
Mh Ole sendeka akajaribu kuwasihi wakae ili kutafuta muafaka lakini haikuwezekana. Hatua hiyo iliwafaya wabunge wa upinzani wasimame na kuanza kuimba nyimbo za kuwataka wezi watoke ndani ya ukumbi wa Bunge. Na ndipo ikamlazimu Spika wa Bunge kuahirisha Bunge mpaka watakapojadiliana.
Picha: Matukio na Vijana
0 maoni:
Post a Comment