Bunge la Uganda limepitisha muswada wa kuondoa ukomo wa umri katika kugombea Urais ambapo ukomo wa umri ulikuwa ni miaka 75.
Bunge hilo pia limerudisha nyuma ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano jambo linaloashiria kwamba wabunge wa sasa wataendelea kushikilia nafasi zao hadi mwaka 2023 kutegemeana na tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa mabadiliko hayo ya Katiba
Mabadiliko hayo ya Katiba yaliyopitishwa kwa kura 315 dhidi ya kura za upinzani 62 yanampa nafasi Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania kiti cha Urais kwa muhula wa sita.
.
0 maoni:
Post a Comment