Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbunge Aliyejiuzulu Ubunge Kinondoni, Autamani Ubunge Tena

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Dar es Salaam kupitia CUF na kisha kujiuzulu ubunge na kujiunga na CCM Bwa Maulid Said Mtulia (pichani) ametangaza nia yake ya kugombea tena ubunge katika Jimbo hilo. 

Kupitia Ukurasa wake wa Facebook ameandika ..
"Kwanza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni.

Pili, nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF.
Tatu, nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu.
Hivyo basi, nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni.
Mimi mtumishi wenu,
Maulid Mtulia."
_____________
>>>>>
KWA UPANDE WETU POLITIKSI KURUNZINI, MBALI NA KUWA HAKI YAKE YA KIKATIBA LAKINI NI DHIHAKA KWA WANANCHI NA KUCHEZEA PESA ZA UMMA. TUNADHANI KUNA ULAZIMA IFIKE MAHALI KUWE NA SHERIA KWA KIONGOZI ALIYECHAGULIWA KAMA ATAJIUZULU KWA KUPENDA MWENYEWE BASI ALIPE NA GHARAMA ZA UCHAGUZI ULIOMPA MADARAKA

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO