Naibu Meya wa jiji la Arusha,Viola Likindikok akiangalia baadhi ya vyombo vinavyopatikana dukani hapo anayefatia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo katikati akifungua duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hiyo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez ( Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi akiingia katika duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAKambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa hizo ,Duka hilo lilifunguliwa juzi eneo la njiro jijini Arusha,kulia ni Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
Kushoto ni Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya Gold Crest ya Mwanza na Arusha Mathias Manga mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa duka kubwa lavifaa mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli linalomilikiwa na kampuni ya kimataifa ya PiMAK
Meneja Mkuu wa kampuni ya PiMAK ya kimataifa inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mapishai kwenye mahoteli akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea duka hilo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akimuonyesha bidhaa za kampuni ya PiMAK mtaja aliyetembelea duka hilo siku ya uzinduzi Bi.Mary Mbajo
Wahudumu wa duka hilo wakiwa na vepeperushi vya kampuni hiyo
Muonekano ndani ya duka hilo
Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo akizungumza mara baada ya kukata utepe,kushoto ni diwani wa kata ya Themi jijini Arusha ,Milance Kinabo
Kulia Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akipozi na wadau katikati ni Maya wa jiji Kalist Lazaro
Mbunge wa Arusha Godbless Lema akiteta jambo na wadau wa kampuni hiyo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez akitoa maelezo kwa mteja
Wageni waliofika katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo
Na Pamela Mollel,Arusha
KAMPUNI ya kimataifa ya PiMAK inayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya mbalimbali vya mapishi kwenye mahoteli , imefungua duka kubwa jijini Arusha kwaajili ya kuwarahisishia watumiaji wa vyombo hivyo kuvipata kwa wakati
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo la kisasa Makamu Mwenyekiti TATO Henry Kimambo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwepo kwa duka hilo hapa Tanzania tayari ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara wa mahoteli
Kimambo alisema kuwa kampuni ya PiMAK kuja kuwekeza nchini itasaidia ajira lakini pia kuwainua wajasiriamali wadogo wenye ndoto ya kufika mbali
“Kuna hawa wajasiriamali wadogo ambao wanajihusisha na maswala ya upishi watapata fursa ya kutanua biashara zao kwa kuwa tayari vifaa vinapatikana kiurahisi”alisema Kimambo
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Ali Donmez alisema, kampuni hiyo yenye makao yake Uturuki imeamua kufungua maduka hapa Nchini Tanzania kwaajili ya kuwarahisishia wateja wake ambao walikuwa wakiagiza vyombo hivyo nje ya nchi
Akizungumzia kuhusiana na bidhaa hizo, alisema kuwa ni bidhaa kwa ajili ya matumizi ya hoteli, migahawa na huduma kubwa za mapishi vikiwamo vya kukatia nyama, kuhokea mikate, kuoshea vyombo, kupikia na huduma nyingine za kihoteli
CREDIT: JAMII MEDIA, ARUSHA
About Ujenzi Connekt
SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
0 maoni:
Post a Comment