NA: MWANDISHI WETU ARUSHA
Kongamano la pili la utalii na amani ambalo hushirikisha wanahabari, wanafunzi na wadau wa utalii nchini, linatarajiwa kufanyika mkoani Arusha, Januari 19,2018.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa kongamano hilo la pili kufanyika mkoani hapa, Andrea Ngobole alisema, kongamano hilo, limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Shahanga sports promotion.
Ngobole alisema, lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kupinga vita ujangili na kuhamasisha uhifadhi endelevu ambao utashirikisha jamii.
Alisema katika kongamano hilo,wanahabari watajadili mchango wa vyombo vya habari katika kukuza utalii na vita dhidi ya ujangili pia umuhimu wa jamii kushiriki katika uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.
“kama ilivyokawaida mada mbali mbali zitatolewa na wahifadhi, watafiti katika masuala ya uhifadhi na utalii na pia waandishi wa habari waliobobea katika masuala ya uhifadhi ”alisema.
Alisema kongamano hilo pia litaambatana na mashindano ya riadha ya Tourism Marathon ambayo pia yatafanyika Arusha kuhamasha utalii.
Mkurugenzi wa taasisi ya Alfredo Shahanga promotion, Alfredo Shahanga alisema wanariadha zaidi ya 200 wanatarajiwa kushiriki.
"kwa ujumla kongamano la mashindano hayo ni sehemu ya tamasha la Arusha tourism Festival ambalo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari, wadau wa utalii na wanariadha "alisema
Wanahabari ambao watashiriki kongamano hilo ni kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Dar es Salaam, Mara na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.
Na haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea katika kongamano la mwaka jana hapa mkoani Arusha
0 maoni:
Post a Comment