Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania lazinduliwa Jijini Arusha
Katibu mkuu baraza la Sanaa Tanzania amewataka wazazi na walezi wa hapa nchini kuwalea watoto na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la kwanza la Tanzania Tukuza Utalii Genesis 1,Godfrey Ngereza alisema kuwa tanzania imebarikiwa kwa tunu mbali mbali hivyo watanzania hawana budi kuzitunza na kuzilinda.
Aidha alisema kuwa wazazi hawana budi kuwafundisha watoto uzalendo na kuhakikisha kuwa tamaduni zilizopo haziishi.
"Waswahili walisema samaki mkunje Angali mbichi tukiwalea watoto vizuri ni ngumu kuona maadili yanamomonyoka kwa kuwa tutakuwa tumetengeneza watoto wema" Alisema Godfrey
Kwa upande wake Raisi wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili Tanzania(TAGOANE)Dkt.Godwin Maimu Nnyaka alisema kuwa watoto yatima hawahitaji mavazi na chakula peke yake bali kujengewa msingi bora wa maisha yake.
Dkt.Nnyaka alisema wakati umefika wazazi kuwalea watoto katika misingi ya Imara na kuhakikisha wanakuwa wazalendo.
Aidha alisema kuwa kupitia tamasha hilo litasiadia kujenga vijana wenye hofu ya Mungu na kurejesha uzalendo na maadili kwa vijana.
Nao baadhi ya Washiriki akiwepo mmiliki wa kituo cha faraja Ophanage Faraja Maliaki aliishukuru TAGOANE na kuwataka wadau wengine kuungana na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kuwapa faraja kwa kuwa nao wanastahili kuheshimiwa kama watoto wengine.
Katibu mkuu mtendaji Baraza la sanaa nchini( Basata)Godfrey Mngereza akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo.Picha zote kwa Idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais wa Mtandao wa Wasanii wa wasanii wa Muziki wa Injili Tanzania na maandili nchini Tanzania (TAGOANE) Dkt.Godwin Maimu akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha la Tukuza utalii Tanzania lililozinduliwa rasmi Jijini ArushaPicha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog |
Baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika mazinhira hatarishai na baadae wakachukuliwa na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais wa Tagoane Dkt.Godwin Maimu akiwa anacheza pamoja na watoto katika Tamasha lililoandaliwa la Tukuza Utalii Tanzania lililoandaliwa na Tagoane.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Faraja wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na mlezi Faraja Maliaki,wapo zaidi ya watoto 200 katika ukubi wa Club D Jijini Arusha.
Mgeni rasmi kutoka Baraza la sanaa la Taifa (Basata)Godrey Mngereza akifurahi pamoja na watoto yatima katika tamasha lililoandaliwa na Tagoane Jiiini Arusha.
Wakila chakula pamoja na watoto katika Tamasha
Meza kuu Rais wa Tagoane,Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la Sanaa nchini (Basata)Katibu mkuu Tagoane,na wakurugenzi wa vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es salaam Gifted Wilson akiimba katika uzinduzi wa tamasha la Tukuza Utalii Tanzania Genesis 1 Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog |
Muimbaji wa nyimbo za Injili Miriam Makunja kutoka Arusha akiimba. Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog |
Muimbaji Wolter Chilambo kutoka Jijini Dar es salaam akiwa anaimba katika Tamasha hilo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Hellen Masai akutoka Arusha kiimba .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa akiwa anafurahia kwenye ufunguzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania likilofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus BlogKatibu mkuu mtendaji wa Baraza la sanaa Nchini (Basata)wa kwanza kushoto akiwa pamoja na Rais wa Tagoane katika uzinduzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Watoto wakionyesha mavazi ya ubunifu chini ya Mwanamitindo mbunifu Diana Magesa kutoka Mwanza,Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
0 maoni:
Post a Comment