Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Ahamia Dodoma


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati akiwasili kwenye hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma ya Kigogo pamoja na wasanii wa kikundi cha Hiari ya Moyo Mwinamila wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitamka kukubali karibu ya kuhamia Dodoma akishuhudiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha kwenye makazi yake mapya aliyohamia rasmi mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuhamia kwenye makazi yake mapya Kilimani, mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ataanza kampeni rasmi ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani tarehe 21 ya mwezi huu.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha rasmi mkoani Dodoma ambapo atakuwa akiishi na kufanya majukumu yake ikiwa sehemu ya azma ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya Dodoma Makamo Makuu ya Nchi.

Makamu wa Rais alitoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumrahisishia kuhamia Dodoma pamoja na Waziri Mkuu .

Makamu wa Rais amesema amekuwepo Dodoma kwa siku 11 ambapo amekuwa akishiriki kazi mbali mbali na kuhudhuria vikao vya Chama.

“Tupo Dodoma na Tumehamia rasmi Dodoma, Mwaka mmoja na nusu sasa toka tamko la kuhamia Dodoma limetolewa kuwa ile safari ya Kanani kwa upande wangu leo imetimia”
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliielezea siku ya leo kuwa ni siku ya furaha kubwa kwa Watanzania wote haswa wakazi wa Dodoma.

Waziri Mkuu alimuhakikishia Makamu wa Rais kuwa Dodoma ni nzuri, na wana Dodoma wamefarijika sana na sekta za utoaji huduma za jamii zimetanuliwa.

Waziri Mkuu alisema kuwa Dodoma ni rahisi kufikika na wananchi kutoka kona zote za nchi yetu, hivyo fursa zipo nyingi kwa wananchi wa Dodoma na wa mikoa ya jirani.

Waziri Mkuu alianisha barabara kadhaa ambazo zimekamilika kwa kiwango cha lami na zinazorahisisha usafiri kufika Dodoma lakini pia alizungumzia mradi wa reli mpya ya Standard Gauge ambayo itasaidia usafiri kwa muda mfupi kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo fupi iliohudhuriwa pia na Mawaziri mbali mbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenister Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe, pia Viongozi wastaafu balozi Lusinde na Mzee Ndenjembi walikuwepo kushuhudia Makamu wa Rais kuhamia Dodoma ambapo walimpa jina la kiasili la Mbeleje hivyo Mama Samia hapa Dodoma atafahamika kwa Mama Mbeleje pia.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO