Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NAIBU MEYA ARUSHA MH VIOLA LIKINDIKOKI AONGOZA WAMAMA WA BAWACHA KUADIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI NI NA KUTEMBELEA WAFUNGWA GEREZANI

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mh Viola Lazaro Likindikoki pamoja na kina mama wa Baraza la Wananwake CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini wameadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa kujitolea kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali ya Mt Meru na baadae kutembelea Gereza la Kisongo na kugawa misaada ya kibinadamu kwa wafungwa.

Pichani Mh Viola akiwa na timu yake ya BAWACHA katika piha ya pamoja na maofisa wa Gereza la Kisongo wakiwa na baadhi ya bidhaa walizopelekea wafungwa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani hii leo.

 Naibu Mey wa Jiji la Arusha, Mh Viola Likindikoki (kulia) akishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mt meru kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Olorieni, ambaye pia ni mwanachama wa BAWACHA Arusha Mjini Mama Sabina Francis (mwenye tisheti nyeupe) akishiriki zoezi la kufanya usafi Hopsitali ya Mt Meru kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. 

Naibu Meya Mh Viola Lazaro na Diwani mwenzake Sabina Francis wakishiriki usafiWashirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO