Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA


Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua jambo huko Msoga Mkoani Pwani.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, MarehemuMzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi, 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Muskumu Bwana Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayang Bw. Khamis Mgeja akiongea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016PICHA NA IKULU
Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
Kada wa Chadema Hamis Mgeja akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.PICHA NA IKULU
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO