Aliyekuwa mgombea uteuzi wa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Mh Edward Lowassa ametangaza rasmi hii leo kuwa ndio siku ambayo amejiondoa CCM na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Ametangaza jioni hii katika mkutano mkubwa na waandishi wa habari.
Mbele ya wanaUKAWA na waandishi wa habari katika hoteli ya bahari Beach, Lowassa amesema nia yake ya kuwania uarais wa chi ili kuwaletea wananchi mabadiliko bado iko pale pale.
"Kuanzia leo naondoka CCM, nitikia wito wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.. niungane nao katika kuleta mabadiliko. Namshukuru sana James Mbatia.
Sikufanya uamuzi huu kwa pupa. Nimejiridhisha ndani ya UKAWA ndio kuna fursa pekee kushinda uchaguzi.. tutaondoa uhodhi wa chama kimoja.
(akimnukuu Nyerere) ...CCM sio Baba wala Mama Yangu.. wanaCCM kama wanataka mabadiliko wayatafute nje ya CCM, na mimi CCM sio Baba wala Mama yangu"
Baadae akagusia swala la Richmond na shutuma za ufisadi dhidi yake ambapo alisema watu waache kupiga kelele na kwamba kama kuna mwenye ushahidi aupeleke mahakamani, yeye anajiamini ni msafi.
Aliulizwa maswali mawili na Mwandishi Balile ambapo mojawapo lilihoji kama anampango wa kulipiza kisasi akasema yeye ni mkristo na anasamehe saba mara sabaini na kwamba kama kuna mtu anawasa kulipiziwa kisasi amuombe Mungu wake amsamehe. Akaongezea na kuhoji kwanini watu wawe na mashaka, wamekosea nini mpaka wawe na hofu ya kulipiziwa kisasi?
**
Nao viongozi wengine wa UKAWA walipopewa nafasi ya kuzungumza walisema haya
NLD : Emmanuel Makaidi
Nampongeza Lowassa kwa kuchagua njia iliyosahihi!
CUF: Juma Duni Haji
Sisi chama cha wananchi CUF tunaona ufahari sana kwa maana tumeongeza nguvu kwenye UKAWA kuikabili CCM ambacho kimesahau kabisa hata malengo ya kudai uhuru.. let us go bac to basics; kuondoa maradhi, ujinga na umasikini
NCCR: James Mbatia
Watanzania wameshinda mtihani wa kwanza. Na sisi tunahahidi tutajitahidi usiku na mchana kuhakikisha Tanzania bila CCM inawezekana. Watanzania wajiunge na UKAWA ndilo tumaini hai. Nikupongeze Lowassa na familia yako kwa ujasiri uliouonesha na historia itakukumbuka. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama wasimamie mchakato huu kwa haki..kamwe wasijaribu kufanya kazi ya kuisaidia CCM. Mabadiliko ya mwaka huu sio ndani ya CCM tena.
CHADEMA: Freeman Mbowe
Kwa haya yanayotokea sasa, mazingira ya CCM kudominate Bunge itakuwa historia. Kuwa na Bunge lenye absolute majority, sio sheria za gesi tu, hata bajeti, maazimio n.k..CCM imekuwa ikiangalia zaidi maslahi ya cham badala taifa kwa wingi wao. Sasa itakuwa historia.
Hatujampokea Lowassa pekee. Tumempokea na mamilioni ya watanzania.
Nitakuwa mwendawazimu uacha kumpokea kiongozi mkubwa kama Lowassa ambaye ana mamilioni ya watanzania wanaomuamini na zaidi ya 3/4 ya wabunge wa CCM.
MwanaChadema asiyetuelewa leo tunamuombea kwa Mungu baadae atatuelewa.
Chama cha siasa ni watu.
Ukawa haifikirii kuibadilisha nchi hii kwa kulipiza kisasi.. hofu ya nini?
Tunakushukuru Lowassa kwa kujiamini, umefungua minyororo mingi ya hofu. Umeondoa hofu katika taifa hili.
Chadema haiongozwi na kauli za Mbowe au kiongozi yeyote. Kinaongozwa na Katiba ambayo ina Kanuni, Maadili na Miiko kwa Viongozi.
Ndani ya Chadema aliyeingia mwaka 1992 wakati kinaanzishwa na aliyeingia leo wote wana haki sawa. Msiwanyanyapae wala kuwagopoga wageni eti watakuja kuchukua nafasi zenu. Hatuna nafasi za kugawana tuna wajibu wa kugawana.
Wapo watu tuliowatukana huko nyuma, ni busara tukaombana radhi. Na kwa wale tulioongea ya kweli wawe jasiri kuyarusha na upande waliotoka
Namshkuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa dhati kabisa.. Idara yetu ya Uenezi haijafanya kazi kama Kikwete kuujenga upinzani kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba 2015.
0 maoni:
Post a Comment