Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA Wilaya ya Arusha, Ndg Noel Olevaroya akikabidhiwa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge na afisa wa Chadema Arusha Mjini Ng Bahati Kitumbwizi. Baadae alifanya mkutano na waandishi wa habari.
*********************
Joto la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mkoani Arusha hasa kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini limeanza kupanda upande wa Chadema ambapo makada wake wameanza kuchukua fomu na kurudisha wakiwania kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi Oktoba.
Mtifuano wa kuwania nafasi za uteuzi haupo tu CCM kama ilivyokuwa imezoeleka, sasa hivi vyama vingine vya Upinzani na hasa CHADEMA nao wameingia kwenye vinyang’anyiro. Wanachama wanajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za kuteuliwa na chama hicho kukiwakilisha.
Taayari makada wawili wa CHADEMA wameshachukua fomu za kuwania uteuzi wa kuwakilisha chama kwenye Ubunge Arusha Mjini, wakijaribu “kupimana ubavu” Mbunge anayemaliza muda wake Mh Lema ambaye japo hajachukua fomu bado lakini ameshatangaza nia ya kutetea kiti chake kwa duru la pili.
Makada hao waliojitokeza ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana Wilaya, Mh Noel Olevaroya (pichani) na Mweka Hazina wa CHADEMA Jimbo la Arusha Mjini, Mh Nsajigwa Mwakatobe.
Baada ya kupokea fomu yake mapema hii leo, Noel anaeleza haya katika ukurasa wake wa Facebook “ Namshukuru Yehova Mungu mwenye nguvu kwa kuniwezesha siku ya leo kuchukua form ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama changu pendwa Chadema,ndgu zangu Watanzania wenzangu nimepata maswali mengi na wengine hata kunitukana pasipo sababu yoyote kisa kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Arusha mjini naomba niwaeleze jambo moja chama chetu kinaitwa Chama chetu kinaitwa chama cha Demokrasia na maendeleo kwahiyo kutangaza nia sio dhambi hii ndio misingi ya demokrasi na sisi kama CHADEMA ndio wahumini wa Demokrasia ktk Taifa la Tanzania na ndio maana tunahubiri kila siku kuhusu Democracy, hivyo basi Watanzania wenzangu sio vema kumtukana mtu ni bora kuhuliza kama ujui,wewe unayetukana uijui Arusha kama sisi tunavyoijua,mwache Mungu afanye kazi yake ndio utastaajabu uweza mkuu wa Mungu.Kwasababu Mungu anakwenda kujitwalia utukufu kwa namna ya ajabu na Wiseman Noel Olevaroya ndio mpakwa mafuta wa Bwana na Mataifa watastaajabu uweza mkuu wa Bwana,sijakurupuka namaanisha kutoka ndani ya moyo wangu.Bwana pokea sifa,heshima na utukufu, kwaajili ya mtumwa na kijakazi wako Noelnakupenda Yesu kwasababu umeshatenda na zaidi ya kutenda.Usiyeshindwa,ujawahi shindwa,wewe ni Alfa na Omega.Asante Yesu kwakunimilikisha wakazi wa Arusha nashukuru Bwana”
Kwa mujibu wa ratiba ya michakato ya uteuzi wa ndani ya Chadema, uamuzi wa nani atawakilisha Jimbo utaamuliwa Julai 23 mwaka huu kupitia Mkutano Mkuu wa Jimbo kabla ya vikao vya juu vya chama kufanya uamuzi wa mwisho. Ratiba hiyo inaonesha siku hiyo pia kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la Wananwake kupitisha majina ya wagombea wa Ubunge Viti Maalumu.
Siku kadhaa nyuma Lema amewahi kukaririwa akisema hatishwi na wanaotaka kupimana nae nguvu iwe ni ndani ya CHADEMA ama kutoka CCM au vyam vingine.
“Najua watajitokeza wengi kutaka nafasi hii. Wengine ni makada wa chama changu. Katika mfumo wa vyama vingi hatuwezi kuepuka hali hiyo, jambo la msingi ni kwamba wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu nani hasa ana sifa ya kuwa mwakilishi wao. Hata hawa wanaopata ujasiri wa kutangaza nia ni matokeo ya “ujasiri” wangu wa kupambana na mfumo dume uliokuwa umewatenga vijana katika uongozi wa Taifa hili.” alinukuliwa Lema na Mwandishi Paul Sarwat.
Fomu za kuwania Ubunge zinaendelea kutolewa mpaka Julai 19, 2015 zoezi litakapofungwa saa kumi kamili jioni.
0 maoni:
Post a Comment