Mh Godbless Jonathan Lema akizungumza kwa furaha mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za Maoni Jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA) ambaye pia ni Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini kumtangaza kuwa mshindi kwa kupata kura 255 kati ya 274 ambazo ni sawa na 93.06% ya kura zote na kuwashinda Nsajigwa Mwakatobe aliyepata kura 6 (2.18% na Noel Olevaroya aliyejinyakulia kura 13 (4.74%). Kwa mara ya tatu Mh Lema anapata nafasi ya kugombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 na baadae mwaka 2010 aliposhinda na kuwa mbunge kabla ya kuvuliwa ubunge na Mahakama na kurudishiwa tena aliposhinda rufaa.
Lema akitumbukiza kura yake kwenye sanduku la kupigia kura
Mtoto wa Lema akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya baba yake kwa ushindi alioupata
Wakati wakisubiri matokeo yatangazwe
Joyce John Mukya akitoa salamu za shukrani kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Arusha Mjini na BAWACHA mara baada ya kutangazwa kinara wa wagombea ubunge Viti Maalumu kwa Jimbo la Arusha Mjini kwa asilimia 73.06 na kuwaacha mbali washindani wenzake saba.
Tabasamu la furaha baada ya kufahamu ni mshindi
Godbless Lema akisaini fomu za matokeo
Joyce Mukya, mshindi wa kura za maoni Viti Maalumu akisaini fomu ya matokeo
Viola Likindikoki aliyekuwa anawania uteuzi wa Viti Maalumu nae pia akisaini fomu za mtokeo. Viola ni Mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya ya Arusha Mjini
Katibu wa Baraza la Vijana Arusha Mjini Mh Glory Kaaya aliyekuwa pia anawania nafasi ya Viti Maalumu kwa Jimbo la Arusha Mjini akisaini fomu ya matokeo
Grace Macha akihutubia wajumbe na kuwashukuru kwa kura walizompatia japo hazikutosha kumtangaza mshindi
Nsajigwa Mwakatobe akiomba kura kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Jimbo la Arusha Mjini CHADEMA. Kura zake hazikutosha kumtangaza mshindi hata hivyo
Wageni waalikwa wakifuatilia uchaguzi huo
Bosi mzito wa Ausha255 “Noise of Silebce” akiteta jambo na mke wa Mh Lema Bi Neema Lema ukumbini hapo.
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
Ubunge Jimbo la Arusha Mjini
1. Godbless Lema- 255 (93.06%)2. Noel Olevaroya- 13 (4.74%)
3. Nsajigwa Mwakatobe - 6 (2.18%)
Jumla ya Kura - 274
Viti Maalumu Jimbo la Arusha Mjini
1. Viola Likindikoki - 5
2. Flora - 1
3. Theresa Minja - 1
4. Joyce Mukya - 39 (73.6%)
5. Grace Macha - 3
6. Pamela - 0
7. Glory Kaaya - 1
8. Prisca Massawe - 3
0 maoni:
Post a Comment