Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BIDHAA ZA KIDOTI ZATINGA JIJI LA ARUSHA; VIJANA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIJASIRIAMALI

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza



warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti

mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari


Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao

mabalozi wa kidoti   wakiwa kazini

baadhi ya bidhaa zinazosambazwa nakidoti jijini Arusha

hizi ndizo ndala za kidoti

mawigi ya kidoti ndio haya



Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog

Wito umetolewa kwa vijana ndani ya jiji la Arusha kujitokeza katika

kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza

kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya

jamii kukosaa thamani.

Wito huo umetolewa na Joketi Mwigelwa (kidoti) wakati akichagua vijana

wajasiriamali ndani ya jiji la Arusha katika ukumbi wa triple A jijini

hapa ambapo anatarajia kuwapata wajasiriamali vijana ambao

hatawaingiza katika fursa ya wajasiriamali kwa kupitia kampuni yake ya

kidoti.


Alisema  kuwa amevutiwa  kuja kuwekeza ndani ya jiji la Arusha  katika

nyanza za ujasiriamali kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Arusha

hususa ni wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la

ujasiriamali na maendeleo binafsi.


Aidha alibainisha kuwa katika  mchakato huo wanatarajia kupata

wajasiriamali wapatao 13 ambapo tofauti na kujiingizia kipato cha

ujasiriamali pia watakuwa mabalozi wa kutangaza bidhaa zilizo chini ya

kampuni ya kidoti.

“ndugu mwandishi unavyowaona hawa wote hapa ni vijana kutoka mkoa

mzima wa arusha na mikoa ya jirani tunawafanyia usaili na kupata

vijana ambao wanakithi vigezo vya kuingia katika ujasiriamali ,utakao

wapelekea wao kufanya kazi na kampuni ya kidoti pamoja na kujiajiri

binafsi” alisema kidoti


Pamoja na hayo alisema kuwa kampuni hiyo kwa mwaka huu imeamua

makusudi kusogeza huduma za  ikiwemo bidhaa zake katika mikoa ya nje

ya jiji la Dar Es Salaam ili kuwapa furusa watu wa mikoani ambao

walikuwa hawazipati huduma za kidoti.


Kwa upande wa mmoja wa washiriki waliojitokeza katika mchujo huo

Anolia Agustino  alimpomgeza kidoti kwa hatuqa aliofikia ya kuwaajiri

vijana haswa wasiochana kwani   ,jambo hili litawasaidia wanasichana

wengi kupata ajira pamoja na kujiajiri binafsi.


Aidha alisema kuwa  mbali na kupata ajira pia kampuni hii itawasidia

kujifunza ujasiriamali pamoja na kujiajiri binafsi kwani ,bidhaa za

kidoti ni za bei na fuuu na unaweza kuanza kujiajiri kwa kutumia mtaji

mdogo.

Kwa upande wa mshiriki mungine ambaye teari alikuwa amenufaika na

kampuni ya kidoti aliyejitaja kwa jina la Anjela Mushi alisema kuwa

kampuni hii imemsaidia sana kwani alikuwa anakaa nyumbani bila kazi

lakini alivyoona kwenye mtandao wa kijamii aliamua kujitafuta

mawasiliano na kuanza  na mtaji mdogo na kwasasa ivi mtaji wake

umekuwa.


“mimi nilianza kuona bidhaa za kidoti katika mitandao ya kijamii kama

intagramu  nikaamua kutafuta mawasilano kwakeli nilipata na nilikuwa

na mtaji mdogo kwani nilianza na mtaji wa shilingi laki moja na sasa

na shilingi laki nne na biashara yangu nilianza mwezi wa tano na sasa

ni mwezi wa saba  kwa hadi sasa nina mienzi mitatu nashukuru mungu

mtaji wangu umekuwa”alisema Anjela.

Alimalizia kw akumpongeza kidoti na kumsihi aendelee kuwasaidia

wasichana kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto ya ajira kwani ajira

imekuwa ni ngumu

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO