Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UKAWA WASHIRIKI FUTARI YA PAMOJA

 

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD Zanzibar, Ahmad Hemed.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.

Baadhi ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA (Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni) na Mama Riziki.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Vioingozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini) na Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni).

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed akiwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari. Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Vioingozi Wakuu wa UKAWA kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini) na Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni).

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO