BLOGU HII IMEANZISHA MFULULIZO WA UTAMBULISHO WA VIJANA WANASIASA WA MKOA WA ARUSHA NA MIKOA JIRANI ILI UMMA UWEZE KUWAFAHAMU WASIFU, UWEZO NA UZOEFU WAO KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA SIASA ZA TANZANIA. HAWA NI WALE WALIOJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UBUNGE NA UDIWANI. BLOGU HII ITAKUWA INAKUTAMBULISHA KWAKO MWANASIASA MMOJA BAADA YA MWINGINE.
KWA LEO NAMLETA KWENU MWANADADA MACHACHARI KWELIKWELI KUTOKA JIMBO LA HAI MKOANI KILIMANJARO.
Anaitwa Doris Cornel Gillius wengine wanamfahau kwa jina maarufu la Doreen Don au Dodoo
Doris ni mmoja wa wanawake wapambanaji sana katika harakati za Mageuzi Nchini. Alianza siasa akiwa na umri mdogo kabisa wa miaka 9 akiwa chipukizi ndani ya CCM. Aliweza kushika nyadhifa mbalimbali na kubwa ndani ya chama hicho mpaka 2010 alipoamua rasmi kujiunga na jeshi la ukombozi la CHADEMA.
Utumishi ndani ya CHADEMA
Akiwa CHADEMA, alichaguliwa kuwa Mratibu wa uhamasishaji Bavicha Wilaya ya Hai, na baadae akawa Mkufunzi wa Programu ya CHADEMA ni Msingi kwa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.
Doris ni mwanzilishi ya programu mbalimbali za kiharakati Jimboni Hai. Mojawapo zikiwa ni Tweet Chadema Hai na Oparation Unacho mimi na Chadema Damu Damu. Programu zote hizi zilikuwa na mchango mkubwa kwa chama chake.
Uzoefu Kitaifa na Kimataifa
Pamoja na mambo mengine mengi Doris amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi akiwa kama..
- Makamu wa kwanza Mwanamke wa vyuo vya Africa Mashariki (EACSU),
- International Student Social Welfare officer,Oslo Norway,
- Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya vyuo vikuu ikiwemo Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama ambapo alifahamika sana kwa uchapa kazi hata kumpa jina la Mama Mdogo au Rock.
- Pamoja na hayo amewahi kuteuliwa kuwa Balozi wa Tumaini Jema "Goodwill Embassodor kutetea haki za wanaoishi na virusi vya Ukimwi vyuoni.
- Aliwahi kupata medali fedha katika tamasha la wanawake lililoandaliwa na IFM-SO chini ya Bi Hellen Kijo Bisimba kwa kusimamia kidete haki za wanawake vyuoni.
- Amekuwa mratibu wa programu ya kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu kupitia Taasisi ya Mkombozi yenye ofisi zake Mjini Moshi na Arusha.
Kuhusu Wanawake
Doris ni mwanamke aliyependa elimu sana na kuamini elimu ni silaha muhimu ya kumkomboa Mwanamke wa Kitanzania katika maadui watatu wa Taifa hili kama ilivyowahi kufafanuliwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl JuliusNyerere ambao ni ujinga,maradhi na umaskini.
Elimu yake
Doris ni msomi wa Chuo Kikuu ambaye ana shahada (Degree) ya kwanza katika masuala ya jamii na kwasasa anaalizia degree ya pili (Masters) katika Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway.
Historia yake kielimu ni kama inavyojieleza hapa chini. Amesomea kozi nyingi za muda mfupi ndani na nje ya nchi na zote amezifanyia kazi katika kuihudumia jamii ya kitanzania na wanawake na watoto wakiwa wahusika wakuu.
- Alisoma shule ya Msingi Kilimanjaro na kufaulu kwenda Mawenzi Secondary Moshi mpaka kidato cha nne.
- Kidato cha sita alimalizia katika shule ya Seminari ya kisabato ya Ikizu mkoani Mara,na hapo alichaguliwa Chuo cha Ustawi wa Jamii na kumaliza shahada yake ya kwanza ya Kazi Jamii.
- Alijiunga na Chuo cha Oslo and Akershus University cha Norway kwa stashahada (Masters) ya International Social Welfare and Health Policy.
- Pamoja na hayo emesomea kozi nyingine mbalimbali ikiwemo Diploma ya Intercultural Communication Nchini Switzerland,
- Conflict Resolution,
- Child Right and Gender sensitive Programme San Jose Costarica,
- Pia amefanya kazi na mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Mkombozi linashughulika na watoto walio katika mazingira magumu mitaani.
- Alisomea kozi maalumu ya Take Off your Shoes kutoka University of Ulster Uingereza, na Street work course kutika shirika la Street Invest London Uingereza.
Kwa kifupi Doris Cornel Gillius ni mwanaharati mpambanaji, msomi mwenye upeo mkubwa wa kuona mbali, mzoefu wa maswala yanayoihusu jamii yake, mtendaji na asiyeamini katika kushindwa. Zaidi Doris ni mpenda soka na mchezaji mzuri. Kipenzi cha Music wa Reggae na country.
****************
Baada ya kuyafahamu hayo sasa nikushirikishe matukio haya machache ambayo yanaonesha ushiriki wake kwenye siasa za CHADEMA.
Hapa akihutubia wananchi wa Chanika-Rundugai katika Jimbo la Hai (hawaonekani pichani), mwezi Julai mwaka 2012
Hapa Doris Cornel akibadilishana mawazo na Katibu wa Baraza la Vijana CHADEMA Mkoa wa Arusha Bi Jenifer Causerie katika Mkutano wa Uzinduzi wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini
Msisitizo jukwaani
Doris Cornel akikaribishwa kwenye hafla maalumu ya kuwaaga wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha wanachama wa umoja wa vijana wa CHADEMA vyuo vikuu. Hii ilikuwa ni mwaka 2012.
Doris Cornle katika ziara ya kuimarisha chama Kikavu Chini miaka ya 2011/12
Doris Cornel akisaidia zoezi la usaili wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Jimbo la Arusha Mjini mwezi Julai mwaka 2014 alipokuwa amerudi likizo yake ya masomo Norway
Doris Cornel Gillius katika jukwaa la Kampeni za Udiwani Kata ya Them Jijini Arusha mwezi Juni mwaka 2013
Doris Cornel akihutubia wananchi wa eneo la KIA Wilayani Hai (hawaonekani pichani) katika mkutano wa kawaida wa CHADEMA kujiimarisha mwezi Juni mwaka 2012
Vijana wa BAVICHA toka Arusha ambao waliamua kufanya safari kuungana na wenzao wa Hai wakongozwa na Doris Cornel katika mkutano wa kisiasa wa CHADEMA eneo la KIA mwezi Juni 2012. Kutoka kushoto, Hassan Noor, Moses Joseph, Doris Cornely, Zion William, Emmanuel Saro na Bosi Mzito wa blogu hii akiwachombeza mawili matatu.
0 maoni:
Post a Comment