Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Binti wa Michuzi Ajitoa Kimasomaso; Achukua Form ya Ubunge wa Viti Maalum

 

Zahara Michuzi alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.

Zahara Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger na mpiga picha hodari wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamalizia muda wake sasa.

Binti wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi yaChama Cha Mapinduzi.

Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.

Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora

Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.

Zahara (kushoto) akilipia fedha halali ya form hiyo huku mama yake mlezi (katikati) akishuhudia kitendo hicho.

Zahara sasa safari yake ya kuufukuzia ubunge wa viti maalu ndipo ikaanza huku akiipitia form yake kwa mara ya kwanza toka azaliwe

Mwasham (kushoto) akitoa baadhi ya ufafanuzi kwa baadhi ya vipengele vilivyomo katika form hiyo.

Picha zote na aloyson.com TBN

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO