Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Mbunge Nassari amenusurika ajali ya helkopta Jimboni kwake

Habari zilizotufikia jioni hii na kuthibitishwa na Katibu wa Mbunge wa Arumeru Mashariki zinaeleza kuwa Mbubge Joshua Nassari pamoja na abiria wengine wawili na rubani wao wamenusurika kifo baada ya helkopta waliyokuwa wakisafiria kuhamasisha uandikishaji Jimboni kuanguka jioni ya leo.

Taarifa zinaeleza kuwa helkopta hiyo imeanguka katika kijiji cha Leguruki Wilayani Arumeru Mashariki baada ya hali ya hewa kuwa mbaya.

Nassari na majeruhi wengine wamewahishwa hospitali ya Selian Jijini Arusha kwa matibabu ya majeraha kiasi waliyoyapata.

Blog hii inaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na kukujuza kila kitu.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO