Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ben Saanane - Nalaani vikali kauli ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Ndugu Samweli Sitta kutaka kuhujumu Uhuru wa Kujadili mchakato wa Katiba!

BENMbali na Kulaani vikali kauli ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Ndugu Samweli Sitta na Pia agizo la Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Bi.Rehema Nchimbi natoa rai kwa watanzania tujiandae kuchukua hatua kali za kiraia na kisiasa

Ndugu Samweli Sitta ameliambia Bunge Maalumu la Katiba kuwa kuna chombo kimoja cha habari kimekua kikijifanya kuwa kinajua kuandaa midahalo na makongamano sana na kurusha moja kwa moja kwa watazamaji midahalo ambayo washiriki wake wamekua wakilishambulia bunge maalumu la katiba na pia washiriki wanaonekana kuwa wa upande mmoja hivyo akapendekeza serikali iangalie hatua za kuchukua na pia akamtaja waziri wa Habari kwa jina lake.

Kauli hii ya Samweli Sitta inaonekana kukilenga waziwazi kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One Stereo.

Hivi ni vitisho si kwa chombo hiki tu bali kwa tasnia nzima ya habari inayoongozwa na sheria mbovu ikiwemo ile sheria ya magazeti ya mwaka 1976.

Ni kinyume cha katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 18(1) inayotoa uhuru wa kutoa maoni,uhuru wa kutoa na kupokea habari. Mwenyekiti wa Bunge la katiba lililopewa jukumu la kuboresha rasimu ya sheria mama ya nchi(Katiba) anaongoza kwa kutoa matamshi yanayovunja sheria mama iliyopo(Katiba ya Sasa)?

Mathalani,Rasimu ya katiba mpya hasa ibara ya 30 imelinda uhuru wa Maoni,Ibara ya 31 imelinda uhuru wa Habari na vyombo vya habari na pia ibara ya 34 ya Rasimu imelinda Uhuru wa mikusanyiko na kushirikiana na wengine.Ibara zote hizi zimeshambuliwa na Mwenyekiti wa Bunge maalumu la katiba akiungwa mkono na baadhi ya wajumbe ambao wanatokea kwenye tasnia ya habari akiwemo Ndugu Hamis Dambaya.Ni jambo la kusikitisha na la aibu kwa taifa linalolenga ustawi wa kidemokrasia katika karne hii iliyostaarabika

Sitaki kuamini kuwa Ndugu Sitta amekua ignorant kiasi hiki kushindwa kuelewa kuwa midahalo hiyo imekua ikitangazwa kuhamasisha washiriki bila kujali itikadi za kisiasa na pia waandaaji wa midahalo hulipia muda wa matangazo(Air time) kwa vyombo hivi bila kuvunja sheria za nchi.Mtu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (Tanzania Investment Center)Nchini ameonekana kuwa mbumbumbu wa kutisha kuhusu suala la uwekezaji kwenye vyombo vya habari ambavyo vina leseni ya kufanya biashara bila kuvunja sheria za nchi?Pengine kwa fikra zake finyu ndio maana enzi za uongozi wake katika kituo cha Uwekezaji nchi iliingia katika uwekezaji holela na wa kutisha unaoligharimu taifa hadi sasa

Vyombo vinavyomilikiwa na watu au taasisi binafsi kwa kiwango kikubwa vimejitahidi kutoa habari bila upendeleo tofauti na vile vya serikali vinavyotumika kama vyombo vya propaganda kwa serikali na chama tawala kama ilivyo kwa kituo cha Televisheni cha TBC1 kinachofadhiliwa kwa kodi za watanzania

Inasikitisha zaidi kuona mtu ambaye hivi karibuni amekua akijinasibu kuwa na matamanio /uwezo kuwa Rais wa Tanzania akigeuka kuwa adui namba moja wa haki za kiraia na uhuru wa vyombo vya habari.Dikteta anayejiandaa kuishambulia Demokrasia huyu(Assault on Democracy).

Ni katika mazingira haya haya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepiga marufuku mijadala inayolenga kujadili lolote kuhusu bunge la katiba mjini Dodoma.Haya ni matumizi mabaya ya Madaraka na ukiukwaji wa sheria za nchi na uvunjaji wa katiba ya sasa na pia dhihaka kwa maudhui ya rasimu ya katiba

Madikteta hawapendi midahalo na mijadala inayoamsha fikra mpya za kimapambano katika mazingira ambayo uongo unaofadhiliwa na serikali(State Sponsored lies) umeshika hatamu.Madikteta wote duniani hutishwa na na mijadala ya kisomi kwa kuwa madikteta ni wavivu pia wa kufikiri kwa mapana(Critical Thinking).Ni katika mazingira haya ya woga sheria mbovu ya vyombo vya habari hutumika vibaya na watawala ikiwemo mbinu za kishetani za kuteka na hata kuua wanahabari,wanaharakati,wanasiasa na hata wasomi wasiopenda kuburuzwa na watawala.Rangi zao halisi tumeebdelea kuzishuhudia leo hii.Tusirudi nyuma,tushikilie hapa hapa

Na sasa Tujiandae kukabiliana vikali na utekelezwaji wowote wa kauli hizi za kiimla .Tujiandae kulinda katiba ya nchi na haki ya watanzania kwa njia zozote ikiwa ni pamoja na maandamano na migomo

Uhuru wa vyombo vya habari unawambwa msalabani,Haki za kirai na Demokrasia inanyongwa na maimla.Tujitetetee,tujilinde sasa.

MAKALA HII FUPI IMEANDIKWA NA BEN SAANANE (PICHANI)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO