Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HABARI PICHA-WATAALAMU WA UMEME WAKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAISHIO VIJIJINI JUU YA MPANGO WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

SSA51115Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO Arusha,Benedict Nkini (wakwanza kulia) akifafanua jambo juu ya kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,kulia ni Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa hicho ,pia  walizungumza na wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido uliofadhiliwa na REA , lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.


SSA51059Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya katika nyumba  kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,wakati akizungumza na wananchi  wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido unaofadhiliwa na REA  lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.

Picha na Ferdinand Shayo

VIJIJI 120 KUFIKIWA NA UMEME

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Vijiji 120 vilivyopo mkoa wa Arusha vinatarajia kufikiwa na huduma ya umeme kupitia mpango wa kusambaza umeme vijijini unaofadhiliwa na (REA) na kutekelezwa na shirika la umeme la taifa (TANESCO).

Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO Arusha,Benedict Nkini amesema kuwa wako katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo wa umeme vijijini na kwasasa wanaelekea katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.

Benedict Nkini akizungumza katika mkutano na Wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini amesema kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mradi huo ili waweze kujiandaa kuunganishwa na huduma hiyo na pia amewataka waepuke vishoka ambao hutumia uelewa mdogo wa wananchi kujinufaisha.

Afisa Masoko wa Tanesco,Adelina Lyakurwa amesema kuwa amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kuunganishiwa umeme huo wa bei nafuu ambao Mtanzania wa hali ya chini anaweza kuumudu ,ambapo Mwanakijiji atatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi 32900 ili aweze kuunganishiwa umeme.

“Tunawaunganishia umeme watu wote wenye nyumba za mawe,matofali,mbao kwa hiyo tunawaomba wananchi watoe ushirikiano ili kufanikisha mradi huu,kwa upande wa nyumba za nyasi na makuti kunahitajika ushauri wa kitaalamu kwasababu za kiutaalamu ili kuepuka moto ambao unaweza kutokea kutokana na hitilifu ndogo” Alisema Afisa Masoko

Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO wilaya ya Monduli ,Ramadhani Mkayala amewataka wananchi watafute wakandarasi wazuri waliodhinishwa na shirika ili kuepuka vihatarishi vya moto

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Monduli Sophia Mligo wa kijiji cha Miserani na Gasper Lengta wamesema kuwa wameupokea mpango huo vizuri na kuwaomba TANESCO wazidi kufanya ushirikishaji zaidi na wananchi ili uweze kufanikiwa bila vikwazo.

“Kuna wakati tulihisi kuwa serikali imetusahau watu wa vijijini lakini sasa tunafarijika kuona hawa REA na TANESCO wanakuja kutuunganishia umeme na tayari wameanza kuchimba mashimo kwenye kijiji chetu shughuli iliyobaki ni kufukia nguzo ,uhakiki ulishafanyika hapo awali” Alisema Parirong’o Sipitieki ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ingoikumeni.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO