Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JK: TUNAKWAMISHWA NA UZALISHAJI NA MATUMIZI MADOGO MNO YA UMEME

o6

o1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti 6, 2014

o3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

o2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

o4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

o5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

o6

 o7

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

o8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014

oo1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakipata picha ya kumbukumbu na mwenyeji wao Rais Barak Obama wa Marekani wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

oo3

Viongozi wa Afrika wakisalimiana kwa furaha baada ya kupata picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

……………………………………………………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.
Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakati alipozungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo.
Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bila ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika halitatoka kwenye uduni.
Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan African Countries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni asilimia 31 tu na hivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani.
Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umeme ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi wa Bara hilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila raia wa Marekani anatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati 440.
Ameongeza Rais Kikwete: “Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”
Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tu ya Ulaya – Hispania. Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa Afrika zina uwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho kinazalishwa na nchi moja tu ya Marekani Kusini ya Argentina.”
Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi zisizokuwa za kiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu, ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa kilimo.
Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi wa Tanzania.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
07 Agosti, 2014

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO