Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mansour Kusota Rumande!

mansoor

Aliyekuwa Mwakilishhi wa jimbo la Kiembe samaki kupitia tikate ya CCM ambae pia amewahi kuwa Waziri wa zamani wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mansour Yussuf Himid amepandishwa katika mahkama ya Mkoa Vuga iliopo ndani ya manispaa ya mji wa Unguja akikabiliwa na tuhuma za makosa matatu ikiwemo kukutwa na silaha, risasi na marisau.

Wakati akisomewa mmashitaka hayo mwendesha mashitaka kutoka ofisis ya Mkurugenzi wa mashitaka( DPP) Maulid Ali amesema mtuhumiwa huyo mnamo Agosti 2, mwaka huu majira ya saa 7.18 huko nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar alikutwa na silaha aina ya pistol (Director) yenye namba F76172 W.

Kitendo hicho cha kumiliki silaha kimedaiwa mahkamani hapo kuwa ni kwenda kinyume na kifungu cha sheria no 6(3) na 34 (1) (2) cha sheria ya silaha na risasi No 2 ya mwaka 1991 sura ya 223 sheria ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania.

Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kupatikana na risasi za moto 295 za pistol jambo ambalo pia ni ni kosa kisheria.

Aidha Kosa la tatu ni kupatikana na marisau 112 ya bunduki aina ya short gurn( gobore) baada ya marisau 50 aliyotakiwa kuwa nayo kisheria.

Kwa upande wake mtuhumiwa Mansour aliyakana makosa yote hayo matatu aliyosomewa Mahakamani hapo.

Naye Mwendesha mashitaka wa serikali Maulid Ali aliomba mahakama ipange siku nyengine ya kutajwa kesi hiyo kwani ushahidi bado haujakamilika.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Khamis Ramadhani ameiambia mahakama hiyo kuwa makosa mawili ya mtuhumiwa yana dhamana lakini kosa moja la kukutwa na silaha halina dhamana.

Wakili wa mtuhumiwa,Mansour Gasper Nyika amedai mahakamani hapo kuwa wanakusudia kupeleka ombi la dhamna katika Mahkama kuu Zanzibar.

Hata hivyo Hakimu Khamis ameiakhirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 mwaka huu kwa kutajwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi tarehe hio wakati kesi yake itakapotajwa tena

 

Chanzo: Mazrui Media & Communication

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO