Ikiwa vuguvugu la chaguzi za Kitaifa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo likiwa linaanza kupamba moto, hususani kwa Baraza la Vijana (BAVICHA) ambapo fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika baraza hilo zimeanza kutolewa tangia Agosti 10 mwaka huu, Mwenyeiti wa Vijana wa chama hiicho Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Diwani wa Levolosi Jijini hapa Mh Ephata Nanyaro amejitokeza kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Taifa wa Baraza hilo.
Akizungumza na Blog hii, Nyanyaro amethibitisha kuchukua fomu hizo katika ofisi za Chadema Kanda ya Kaskazini na kwamba atashiriki katika uchaguzi huo kwa mujibu wa taratibu za chama kwasababu ana sifa na vigezo vinavyohitajika.
Ifuatayo ni sehemu ya Wasifu wa Ephata Nanyaro katika siasa za Tanzania (Maelezo ya wasifu huu ni kwa mujibu wa vyanzo vyetu). Blog hii itakuwa ikirusha wasifu wa kila mgombea anyejitokeza kwa kadiri taarifa zake zitakavyopatikana.
- Ni kijana mwenye shahada ya kwanza
- Ni kijana mpole lakini machachari, mwenye uwezo wa kuwaunganisha vijana, mchapakazi anayejimudu kila idara, ana maadili mema yasiyotia shaka, ana dhamira njema juu ya chama, anakijua chama kwa udhati na undani wake.
- Ni Diwani wa kata ya Levolosi, Arusha mjini. Ikumbukwe ni kati ya madiwani Arusha waliokataa rushwa kipindi kile cha mpasuko Arusha. Hawakuingia kwenye vikao vya Manispaa kwa muda mrefu.
- Ni Mwenyekiti BAVICHA Mkoa wa Arusha
- Ni Mwenyekiti wa Wilaya aliyemaliza muda wake hivi karibuni
- Mwenyekiti BAVICHA aliyemaliza muda wake Wilaya ya Arusha Mjini.
- Alipinga Ufisadi katika uzinduzi wa Jiji la Arusha.
- Ameshiriki kazi mbalimbali za chama kama chaguzi za Kiteto, Biharamulo, Igunga, Arumeru, Kalenga, na chaguzi za Kata mbalimbali za Arusha( Kata mbili za CCM zimekuwa za Chadema, na kata 4
- zilikombolewa na Chadema yeye akiwa Mwenyekiti wa Wilaya). Kilimanjaro na Tanga. Sifa za ziada
- Ameoa na ana watoto
- Ni Mcha Mungu.
- Ana certificate ya Campaign for Change.
0 maoni:
Post a Comment