Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KOICA/KAAT) yapata uongozi mpya *Wadhamiria kuitangaza Tanzania kibiashara kimataifa

Na Saidi Mkabakuli

Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya, utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa muda wa miaka miwili.

Waliochaguliwa kuongoza KAAT ni pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara). Katika nafasi ya Uweka Muweka Hazina, aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini wa Mama Anna Mkapa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw. Katemba ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za Kimataifa, amesema kuwa Tanzania ina fursa kubwa katika eneo la biashara za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali zilizopo nchini na kuchagiza kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa kujitangaza tu.

Bw. Katemba aliongeza kuwa kama Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na kuwa mabalozi wazuri, Tanzania itakuwa na uhakika wa kukamata masoko makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa ujumla.

“Kwa mfano kwa mujibu wa hali ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo wa biashara ya bidhaa na huduma nje haukuwa wa  kuridhisha ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilipungua kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni 8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola milioni 8,532.0,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Katemba kuwa ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi, Tanzania haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho la Biashara Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi wanachama kuboresha biashara zao.

“Katika kikao cha tisa cha WTO, Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana

kuwa na “Mpango wa Bali” ambao unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi ya kuzalisha chakula cha akiba, kuinua kiwango cha biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya nchi changa kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza bidhaa zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” alifafanua.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim alisema kuwa Tanzania ina bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea na kutolea mfano mchele wa Kyela kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.

DSC06190

Rais Mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT), Bw. Stephen Katemba (Kulia) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa. Anayemsikiliza ni Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Kushoto).

DSC06196

Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo.

DSC06205

Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Muweka Hazina mpya.

DSC06213

Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw. Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar). Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.

DSC06237

Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Wapili kulia).

DSC06244

Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO