Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU UFADHILI WA MIRADI YA MAENDELEO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA JAPAN KWA MWAKA 2014/2015

DSC06295

Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili kushoto) akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15. Majadiliano hayo yalifanyika Julai 25, 2014 katika ukumbi  wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

DSC06300

Wajumbe wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.

DSC06279

Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.

DSC06282

Baadhi ya wajumbe kutoka Tume ya Mipango, Klasta ya Biashara ya Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi ambao walioshiriki kuratibu majadiliano hayo kutoka kulia Bw. Robert Senya na Bi. Sudah Lulandala wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo.

DSC06286

Wajumbe kutoka Serikali ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa Majadiliano ulipokuwa ukiendelea. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.

 

DSC06265

Wajumbe wa mkutano wakimsiliza Mwenyekiti wa mjadala Dkt. Philip Mpango. Upande wa kulia ni wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na upande wa kushoto ni wajumbe kutoka serikali ya Japan.

Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO