Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.

UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.

Nimeamua kuandika kidogo kikombe kisinipite ili kuanika unafiki wa Mwigamba na marafiki zake (Kitila na Zitto), Mwigamba na maswahiba zake (viruka njia wa usaliti) ambao walisaliti ndani ya CHADEMA na baadae kuibuka na uzushi kuwa kipengele cha 6.3.2 (c) kinacho zungumzia muda wa uongozi kwenye katiba ya chama kuwa kimewekwa kinyemela. Kipengele hicho (6.3.2 (c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi"
Mwigamba anasema kipengele hicho kimeongezwa kinyemela huku akijua alishiriki/wameshiriki kwenye kuifanyia mabadiliko katiba ya chama ya 2004 na kuanza kutumika rasmi kwa katiba ya 2006 iliyokuja na kipengele hicho.

Mwigamba pamoja na wajumbe wengine akiwemo rafiki yake (MM) tarehe 13/8/2006 wakiungana na wajumbe wengine wa mkutano mkuu kwa pamoja walisema "...Sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumeamua kuifanyia mabadiliko katiba ya 2004 ya chama chetu cha siasa kinachoitwa CHADEMA ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya nguvu na mamlaka ya umma na dira na dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya chama...". Mwigamba na Zitto walitamka kwa pamoja maneno hayo wakiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo.

Msijiulize kwa nini kwenye hili nawaongelea wote wakati aliyepeleka malalamiko kwa msajili alikuwa Mwigamba peke yake! ukweli ni kwamba utatu huu wa kisaliti nauongelea pamoja kwenye sakata hili kwa kuwa nyendo zote chafu za kisaliti kwa sasa huwezi kuwatenga! Wanaruka pamoja, wanakutana na kupanga pamoja na mawasiliano yao makubwa pamoja na mataniboi wao wa kisiasa ni kuidhoofisha CHADEMA kuliko kuimarisha chama chao kinacho undwa na viongozi walio saliti CHADEMA. Uhakika nilio kuwa nao, watashindwa kama walivyo shindwa kupitia walicho kiita "Mkakati wa mabadiliko 2013".

Mwigamba kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 2/7/2014 alinukuliwa akimshukuru Mungu kwa ofisi ya msajili kwa alicho kiita "..kusimamia na kueleza ukweli wanachama wa CHADEMA kuhusu kuondolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka.." akanukuliwa zaidi akisema "...CHADEMA walinifukuza uwanachama wakiamini kuwa hoja ya kuvunja katiba niliyo iwasilisha kwa msajili itatupwa na hatimaye amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..."


Maelezo ya Mwigamba yamejaa unafiki na hadaa zilizotawaliwa na dhambi ya usaliti! Usaliti wa kukisaliti CHADEMA na sasa anajisaliti na yeye mwenyewe! Hebu msome katikati ya mstari hapa "...hatimaye msajili amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..." utadhani marekebisho hayo yamefanyika yeye akiwa tayari kashasaliti na kwenda ACT!
Kuna haja watu wajue, huyu Mwigamba alikuwa nani ndani ya CHADEMA kabla ya kufukuzwa chamani kwa dhambi ya usaliti kupitia mkakati wa mabadiliko na unafiki wa kumsifu mwenyekiti Mbowe kwa kuendesha chama kwa ufanisi na ubunifu kwenye mkutano wa kanda ya kaskazini pale Corridor Spring (Arusha) Novemba 2013 akiwa anawasilisha ripoti ya mkoa wake (Arusha) huku robo saa baadae akimkashifu na kumtukana Mh Mbowe kupitia akaunti yake bandia ya 'Mkulima maskini' kwenye mtandao wa jamiiforums.
Mwigamba alikuwa nani kabla ya kusaliti CHADEMA?


1. Mwigamba aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha mpaka alipo vuliwa nafasi zake zote za uongozi Novemba 2013.

2. Aliwahi kuwa mhasibu wa chama makao makuu kuanzia 2011 hadi 2012 alipo simamishwa kazi na makao makuu kutokana na matatizo mbalimbali moja kubwa likiwa kushindwa kuleta ripoti ya matumizi ya fedha alizopewa wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambapo zaidi ya milioni 210 zilitumika.


3. Alishiriki kwenye mkutano mkuu wa tarehe 13/08/2006 uliopitisha mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2006 akiwa mjumbe kutoka mkoa wa Arusha (kwa mujibu wa kumbukumbu za mahudhurio).


4. Amekuwa mjumbe wa vikao vya baraza kuu la chama toka 2009 alipo chaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha na amekuwa akishiriki vikao mpaka Nov 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.


5. Amekuwa mjumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa chama toka 2006 na amekuwa akishiriki kwenye mikutano mikuu mpaka Novemba 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.
Lakini kubwa la muhimu ni kwamba, yeye na Kitila Mkumbo ndio walikuwa wanamtandao wakubwa na waandaji wa mkakati wa mabadiliko 2013 kinyume na maadili, itifaki, miongozo na katiba ya chama kwa ajili ya rafiki wao anaye kamilisha UTATU wao wa wasaliti. Lakini pia hawaja wahi kulalamika kwenye kikao chochote kuhusiana na kipengele cha ukomo wa ungozi ndani ya kikao chochote cha kikatiba.

Usaliti na hadaa za Samson Mwigamba na utatu wao wa kisaliti ni upi?!
Pamoja na kujua kuwa alishiriki mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ya chama yeye na rafiki yake anajua kuwa:
1.0 wapo viongozi ndani ya CHADEMA ambao waliweza kuwa na haki ya kugombea na walichaguliwa upya kwa zaidi ya vipindi viwili na hakuja wahi kuwa na mgogoro kwani katiba ya chama ilifuatwa kwa ukamilifu wake.

Viongozi hao ni nani na wanatokea mikoa na kanda ipi?
1.1. Alhaji Ramadhani Kasisiko - mwenyekiti wa mkoa wa Kigoma na rafiki mkubwa wa Zito Kabwe. (Inasemekana hata Hijjah alimpeleka yeye).

1.2. Kansa Mbarouk - mwenyekiti wa mkoa Tabora, huyu ni ndugu na Athuman Balozi (Tabora) aliyesoma tamko fake la waliojiita wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu pale Lamada Hotel na baadae wakaandamana kwenda kwa msajili na CAG.


1.3. Msafiri Wamalwa - Katibu mkoa wa Kigoma.
Viongozi hawa wote watatu hapo juu wanatokea kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) ambako pia ni kanda aliyokuwa anatoka MM na Mzee Said Arfi.
Kwa maana hiyo, kama Mwigamba angekuwa na dhamira safi angemuuliza rafiki yake wa makakati wa mabadiliko aliyempa jina la MM au ange muuliza mzee Said Arfi uhalali wa viongozi hao ambao walichaguliwa zadi ya vipindi viwili.


2.0. Kama dhamira ya Mwigamba ingekuwa haiteswi na dhambi ya usaliti angejiuliza uhalali wa viongozi wengine ambao ni


2.1. Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida na rafiki wa MM ambaye anaitwa
Nobert Kitundu japo alikuja kujiuzuru kutoka na sakata la MM (huyu baadae aliomba kurudi kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kukiri kuwa alipewa hela ili ajiuzuru kwenye ule upepo wa kujiuzuru ambao baadae ulikwama).

2.2. Mwingine ni Mzee Stephen Massawe wa mkoa wa Dodoma ambaye mpaka sasa ni katibu wa mkoa wa Dodoma na alipasifa za kugombea tena baada ya mabadiliko ya katiba 2006 ambayo Mwigamba naye alishiriki mchakato wa mabadiliko yake.

Viongozi wote hapo juu wanatokea kanda ya kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, kanda ambayo anatokea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mwigamba waliye shirikiana kuandaa mkakati wa mabadiliki 2013 na ndio wanaunda utatu wa kisaliti wakishirikiana na MM.
Kama Mwigamba hakuwa na nia ovu, kilicho mzuia asimuulize rafiki yake kwenye utatu wa kisaliti (Dr Kitila) ni nini?!

Itoshe kusema kuwa, pamoja na viongozi hao hapo juu lakini pia wapo viongozi wengine kama marehemu Philiph Magadula Shilembi ambaye naye alishika uongozi kwa kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili, kama mtakumbuka huyu marehemu alisha wahi kuandikiwa makala nzuri sana na MM na Mwigamba mara baada ya kifo chake. Yupo pia mzee Shilungushela kutoka Shinyanga ambaye pia mwenyekiti taifa baraza la wazee ambaye naye alichaguliwa kwa kipindi cha tatu, Shilembi na Shilungushela wanatokea kanda ya ziwa Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara.


Viongozi wengine walio chaguliwa kwa vipindi zaidi ya viwili ni pamoja na mzee Ndesamburo mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro na Mh Conchester Rwamlaza (MB) ambaye ni katibu wa mkoa wa Kagera.
Nabaki najiuliza?!


1. Kwa nini Mwigamba na utatu wake mtakatifu pamoja na mataniboi wao wa kisiasa hoja yao iwe kwa viongozi wa chama taifa wakati kipengele cha ukomo wa madaraka kama kingekuwepo kingehusu viongozi wote mpaka kwenye ngazi ya misingi, matawi, kata, wilaya na hata mikoa na si mwenyekiti na katibu mkuu taifa pekee?!


2. Kwa nini Dr Slaa ahusishwe na kushambuliwa wakati nafasi yake ya ukatibu mkuu na manaibu wake ni nafasi ya uteuzi na si nafasi ya kugombewa na kupigiwa kura?! Nini kimejificha kumuongelea Dr Slaa na wakati huohuo kumuongelea Mh Mbowe wakati mmoja anapigiwa kura na mwingine anateuliwa?! Kumbuka hata rafiki wa Mwigamba kwenye utatu wa usaliti (MM) hakuchaguliwa bali aliteuliwa na mwenyekiti kwenye miongoni mwa majina yaliyo wasilishwa kwake kwa uteuzi na hivyo akawa naibu katibu mkuu bara.

3. Kwa nini rafiki na collegemates wa MM pale udsm ambaye naye ni rafiki na Sisty Nyahoza ambaye ni mhudumu wa ofisi ya msajili waongee lugha moja na kundi lote la utatu wa usaliti kuhusu kipengele cha ukomo wa uongozi?! Lugha moja wanayoongea nikwa bahati mbaya au kuna ka mpango nyuma ya pazia kampango ambako msajili wa vyama jaji Mutungi amejikuta anaingizwa king na ameshtuka akiwa kwenye kilinge cha tope?!


4. Mbona utatu wa usaliti hauongelei mabadiliko ya bendera ya chama pamoja na mabadiliko makubwa yaliyo huisha mfumo wa chama kizima na wamejikita kwenye kipengele kimoja tu ambacho bado ni halali kama vipengele vingine wasivyo taka kuviongelea vilivyo halali?! Nashangaa kwa nini hawaongelei mabadiliko ya bendera, organisation ya chama pamoja na Redbrigade iliyopigiwa kelele na CCM ambayo haikuwemo kwenye katiba ya 2004?!

5. Kama wameamua kusaliti uwepo wao na ushiriki wao kwenye mabadiliko ya chama wakiwa na akili timamu, nani anaweza kusema kuwa watu hawahawa kuwaita kuwa ni wenye kuungana na kuunda utatu wa usaliti na kuanzisha chama chenye kuundwa na viongozi walio saliti CHADEMA hawapaswi kuitwa kwa jina lingine kuwa wao ni Alliance for Cowards and Traitors yaani kwa kifupi ACT?!

IMEANDIKWA NA: MOHAMED MTOI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO