Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari ameweza kutembelea mji wa Fayetteville-Arkansas na kujionea namna vikao vya Halmashauri za Miji zinavyoendeshwa huku wajumbe wakitanguliza maslahi ya umma kwanza.
Nassari yupo nchini Marekani kwa ziara ya mafunzo kwa viongozi vijana kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Pichani juu anaonekana kwenye picha ya pamoja akiwa na Viongozi vijana wenzake kutoka Afrika; Eric Bukasa Ntumba ( DRC), Piet (Namibia), Dr. Gwamaka Kifukwe PhD(Tanzania), Joshua Nassari ( Tanzania)
Hapa akiwa na Mwakilishi wa Arkansas Bw Grag Leding kupitia chama cha Democrats cha Rais Obama. Akiwa katika mji wa Fayetteville Arkansas, alipata wasaa wa kujifunza mengi toka kwa wenyeji namna wanavyoendesha Serikali za Mitaa. Nassari anaeleza kuwa Mwakilishi Leding alichaguliwa akiwa na miaka 32 tu na hakuwa ameoa. Alikuwa ni mtu wa kawaida asiyefahamika kwenye siasa za mji huo, sifa ambazo zinawiana na namna Nassari alivoibuka na kutwaa Ubunge wa Arumeru Mashariki ambako anafanya uwakilishi mzuri wa wananchi wake Bungeni.
Kwa muda mfupi ambao ametumikia Jimbo la Arumeru Mashariki amweza kufanya mambo mengi ambayo hayakuweza kufanyika kwa miaka mingi chini ya wabunge waliomtangulia, kiasi cha baadhi ya wasiofurahishwa na mafaikio hayo kuendesha mikakati ya siri kumfarakanisha na wananchi. Kwa mfano, kuna taarifa ya hivi karibuni ilimnukuu Mwenyeiti wa Halamashauri ya Meru akikataa kupokea msaada wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shue zilizoko kwenye Kata yake kwasababu zina jina la Mbunge huyo, jambao ambalo alidai atakuwa anamjenga mwenzake kisiasa huku yeye akionekana hajafanya kitu.
0 maoni:
Post a Comment