Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Serikali yapiga ‘stop’ ajira 70 za Uhamiaji

 

  Na Ibrahim Yamola na Beatrice Moses, Mwananchi

Dar es Salaam.

Serikali imesitisha ajira 70 za konstebo na koplo wa Uhamiaji baada ya kuzuka kwa tuhuma za upendeleo uliokithiri wakati wa usaili.

Agizo hilo la Serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil ambaye ametengua kauli yake ikiwa ni wiki mbili tu tangu alipozitangaza nafasi hizo.

Mara baada ya ajira hizo kutangazwa, wadau mbalimbali walianza kulalamika kwa madai kwamba nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo kwa ndugu na marafiki wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isack Nantanga ilisema Abdulwakil amesitisha ajira hizo baada ya kuzagaa kwa tuhuma za upendeleo kwa ndugu na jamaa wa watumishi wa idara hiyo.

“Kutokana na kusitishwa kwa zoezi hili, waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Agosti 5 mwaka huu sasa watatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena.”

Ilisema Abdulwakil ameunda kamati ndogo kuchunguza tuhuma hizo na ikikamilika ndipo uamuzi utakapofanyika.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba kulikuwapo na upendeleo wakati wa usaili.

Julai 13 mwaka huu, Idara ya Uhamiaji ilifanya usaili wa kujaza nafasi 70 za mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waliopita ni 6,115 ambao walichujwa na kufika 1,681 walioingia katika kinyang’anyiro cha kusaka watumishi 70.

Utata ulivyo

Baadhi ya waliotakiwa kuripoti Agosti 5 mwaka huu wanaodaiwa kuwa ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo ambao majina yao yalisambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni: Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Amin Mandemla, Alphonce Kishe – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Aleluya Kishe na Asha Burhani Idd – ndugu wa Ofisa Uhamiaji na Tatu Burhani Idd.

Wengine ni Beatrice Temba – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Joseph Kasike, Geofrey Justine Mhagama – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Rose Mhagama, Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Daniel Mgendi na Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Makwinya.

John Alfred Mungulu – mtoto wa Ofisa, Uhamiaji Alfred Mungulu, Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji, Milambo, Michael J. Choma – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, John Choma, Shimba H Zakayo – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Zakayo Mchele na Upendo E. Mgonja - mtoto wa Ofisa Uhamiaji Mgonja.

Wengine ni Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Adam Kidesu, Elizabeth Edward – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Edward Martin, Ester Mahirane – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Mahirane na Basil Lucian John – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Lucian.

Frank E Kajura- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Kajura, Jacob P. Ulungi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Magnus Ulungi, Janeth John Milinga – ndugu wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Milinga, Janeth R Lukuwi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji Eliza Lukuwi, Joseph N. Yondani – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Mary Yondani.

Leila Khatib Irovya - Mtoto wa Ofisa Uhamiaji Abbas Irovya, Lucian F. Mlula – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Mlula, Neema Kasian Lukosi- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Zubeda Abbas, Pendo D. Gambadu – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Gambadu, Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward Mwenda.

Theresia Ernest Kalunde – mtoto wa Ernest Kalunde, Veronica G Vitalis – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Vitalis Mlay, Victor G. Mlay- mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Vitalis Mlay na Catherine J. Mapunda- mtoto wa Ofisa, Lucy Mapunda.

Uhamiaji wajitetea

Idara ya Uhamiaji imekiri kupokea malalamiko yaliyotolewa dhidi yake.

Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Rosemary Mkandala alisema jana kuwa wamepokea tuhuma hizo na wanazifanyia kazi.

“Ninaomba tu wale ambao walishiriki kwenye usaili huo na wana malalamiko wayawasilishe rasmi ili tuweze kuyafanyia kazi. Suala linachunguzwa sasa na matokeo yake yatabainisha kama kuna ukweli au la,” alisema

 

CHANZO: MWANACHI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO